Sunday, March 31, 2013

TAFAKARI: WATAWALA,VIONGOZI & WAPIGAKURA

Na Butije Hamisi, Mwanza
Kila mtu anaweza kuwa mtawala, lakini si kila mtu anaweza kuwa kiongozi. Kuna viongozi wachache sana duniani huku mataifa mengi yakiwa yamegubikwa na watawala.

Hivi wananchi wanaondamana maeneo mboalimbali duniani kwa lengo la kuwaondoa madarakani viongozi au watawala waliowachagua inamaana wakati wanawachagua hawakuwa makini kwa kile walichokuwa wakikifanya?

Ni wazi kuwa wananchi katika mataifa mengi duniani wamekuwa wakipiga kura kuwachagua watawala au viongozi wao, lakini baada ya muda mfupi huanza kulalama na kuwapinga watawala/viongozi waliowapigia kura wao wenyewe. Swali linalonipa ukakasi hapa nio je, inamaana raia wa mataifa mengi duniani huwa ni mambumbumbu katika utashi wao wa kuamua mtawala au kiongozi wao?

Kuna baadhi ya watu wameshika hatamu kwa njia ya mapinduzi na wakatokea kuwa viongozi na wengine watawala, na ilipofika kwenye uchaguzi wachaguaji waliwapa nafasi na baadae kuanza kulalamika na kufanya maandamano ya kuwaondoa madaraka ambayo mengi yao huleta maafa na uharibifu mkubwa wa rasilimali.

Katiba za mataifa mengi duniani zimeweka kinga kwa mtawala au kiongozi aliyechaguliwa na wanachi. wananchi hao wanakuwa hawana uwezo wa kumtoa madarakani mpaka kipindi chake kiishe au waamue kutumia nguvu. Nguvu ambayo imekuwa ikitumiwa na wananchi  wa mataifa mbalimbali duniani ni maandamano.

Swali la kujiuliza tena hapa ni je, kuandamana kwa lengo la kuwaondoa madarakani viongozi tuliowachagua ndio uamuzi makini/sahihi wa kufika matarajio yale tuliyoyatarajia wakati tukiwachagua watawala/viongozi walioko madarakani? Rejea vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa katika chi za kiarabu.

No comments:

Post a Comment