Saturday, March 30, 2013

RAILA ODINGA AKUBALI KUSHINDWA, AWATAKA WAKENYA KUDUMISHA AMANI



MGOMBEA wa Urais nchini Kenya kwa tiketi ya muungano wa Chama cha CORD Raila Amolo Odinga amekubali kushindwa katika kesi ya kupinga matokeo aliyofungua katika Mahakama ya Juu nchini humo.

Akihutubia taifa hilo muda mfupi uliopita,Odinga amesema kwamba anakubalina na hukumu hiyo iliyosomwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga.

"Nimekubalina na matokeo hayo kwa sababu yakuheshimu Katiba ya Kenya ambayo inasema matokeo ya urais yapingwe katika Mahakama hiyo na maamuzi yatakayotolewa na Mahakama ndiyo ya mwisho"alisema Odiga.

Alisema, "Nilikwenda mahakamani kwa maslahi ya wakenya, hivyo natangaza rasmi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na kuitakia amani serikali iliyoko madarakani,nitashikiana nao katika kujenga nchi yetu".

Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga kutoa hukumu ya kesi hiyo na kusema kwamba mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa huru na uwazi na kumfanya  Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto kuchaguliwa   

No comments:

Post a Comment