Saturday, March 16, 2013

ROONEY AIPAISHA MANCHESTER UNITED …ARSENAL YAICHINJA SWANSEA, LIVERPOOL YAPIGWA 3-1




RIO GRAND ... Ferdinand beats Noel Hunt to the ball
MANCHESTER UNITED wamezidi kujikita kileleni mwa Ligi kuu ya Uingereza baada kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Reading.
Bao hilo pekee lilikuja dakika ya 23 kupitia kwa Wyane Rooney.
Mpira ulianzia kwa Rio Ferdinand aliyepanda na mpira huku akiichambua ngome ya Reading kabla ya kumpa pasi Rooney aliyepiga mkwaju uliombabatiza Pearce na kwenda wavuni.
WAY TO GO ... Rooney opens the scoring after his strike deflects in off Alex Pearce
Rooney akifunga goli pekee
Dakika ya 48 Reading walinyimwa penalti ya wazi baada ya Vidic kumsukuma Mariappa kwenye kisanduku cha hatari lakini kwa mshangao wa wengi refa Mason akauchuna.
Van Persie akakosa nafasi ya kufunga bao la msimu katika dakika ya 90 baada ya kwenda hewani na kuruka tik tak kuunganisha krosi ya Kagawa lakini shuti lake likaenda pembeni.
ASH 'N BURN ... Ashley Young goes down under a challenge from Reading keeper Stuart Taylor
Heka heka langoni mwa Reading
Katika michezo mingine Arsenal iliichapa Swansea 2-0 kupitia magoli ya Nacho Monreal na Gervinho.
Liverpool ikafungwa 3-1 na Southampton huku Aston Villa ikiibuka na ushindi wa 3-2 kwa QPR.
Nayo Stoke City ikiwa nyumbani ikatoka sare ya 0-0 na West Bromwich Albion.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili hii kati Sunderland na Norwich, Tottenham dhidi ya Fulham, Chelsea ikiikaribisha West Ham huku Wigan ikimenyana na Newcastle.

1 comment: