Tuesday, July 15, 2014


Friday, May 16, 2014

DIVISION 4 STOP KUSOMEA UALIMU; WANAFUNZI WATAPEWA MKOPO BILA KUUREJESHA

Serikali imesema ili kukabiliana na tatizo la kuwa na walimu waliofeli mitihani ya sekondari kuanzia mwaka huu itaanza kuwasomesha bure wanafunzi waliofaulu, wanaotaka kwenda kusomea shahada ya elimu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Ulimwengu ya Ufuatiliaji wa Elimu kwa wote iliyoandaliwa na Shirila la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi (Unesco), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema kuanzia sasa wanafunzi waliopata daraja la nne hawataruhusiwa kusomea ualimu.
Alisema ili kuwa na walimu wenye uwezo mkubwa wa kitaaluma na kuondokana na dhana kuwa wanaokwenda kusomea kozi hiyo wameshindwa kupata nafasi sehemu nyingine, wanafunzi waliofaulu watapewa mkopo na Serikali na hawataulipa.
“Ukipata daraja hilo ni kwamba hakuna nafasi ya kujifunza ualimu,” alisema na kuongeza kuwa wanafunzi watakaopata daraja la tatu watapewa mkopo, lakini wao watalazimika kuulipia.
Pia ripoti hiyo iliyoangalia namna mafunzo ya elimu yanavyotolewa imebainisha kuwa walimu wa Tanzania wanaongoza kwa utoro kazini katika Ukanda wa Afrika Mashariki jambo lililochangia wanafunzi kufanya vibaya kwenye matokeo yao ya mitihani.
Akiwasilisha ripoti hiyo, Profesa Galabawa alisema kuna upungufu wa walimu wenye sifa za kufundisha huku taasisi zinazosimamia elimu zikishindwa kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema iwapo Serikali inataka kuwa na walimu wenye sifa zinazotakiwa, italazimika kuwa na Dola 335 milioni (Sh536 bilioni) ambazo ni sawa na asilimia 23 ya fedha yote ya bajeti ya wizara ya elimu mwaka 2011 na kwamba Serikali ibadili utaratibu uliopo sasa wa kutoa elimu.

Tuesday, May 13, 2014

UFAHAM UGONJWA WA MART UNAOSABABISHWA NA PAPILLOMAVIRUS


Warts: Wart: A local growth of the outer layer of the skin (the epidermis) caused by a virus. The virus of warts (a papillomavirus) is transmitted by contact. The contact can be with a wart on someone else or one on oneself (autoinoculation).
Warts that occur on the hands or top of the feet are called "common warts." A wart on the sole (the plantar surface) of the foot is a plantar wart (and can be quite painful). Genital (venereal) warts are located on the genitals and are transmitted by sexual contact; they are a form of STD (sexually transmitted disease).
Warts are nothing new. The word "wart" is from Old English. As far back as the 8th century, a "wart" was, well, a wart.
The medical name for a wart is "verruca", the Latin for wart. A common wart is a "verruca vulgaris". A wart in medicine is also sometimes called by its Spanish name, "verruga".
By now, you probably know that the idea of catching warts from toads is nothing more than an old wives’ tale. But many people still have questions about these unsightly and sometimes painful growths that seem to crop up out of nowhere. Here are WebMD’s answers to 10 frequently asked questions about warts.

How Do You Get Warts?

Warts occur when the virus comes in contact with your skin and causes an infection. Warts are more likely to develop on broken skin, such as picked hangnails or areas nicked by shaving, because the virus is able to enter the top layer of skin through scratches or cuts.
While dermatologists still don’t know why, certain people are more likely to get warts than others. Additionally, children get warts much more often than adults, because their immune systems have not yet built up their defenses against the numerous types of human papillomavirus that exist.

Are Warts Contagious?

Unfortunately, yes. You can get warts from touching a wart on someone else’s body, or by coming in contact with surfaces that touched someone’s warts, such as towels or bathmats.

Can I Spread Warts From One Part of My Body to Another?

Yes, you can. For this reason, it is important not to pick at your warts and to wash your hands promptly and thoroughly any time you touch one of your warts. If you have warts in an area where you shave, keep in mind that shaving over the wart could transfer the virus to the razor and then spread it to other areas of your body.

Why Do Some Warts Have Black Dots in Them?

If you look closely, many skin warts contain a number of black dots that resemble little seeds. These specks are visible blood vessels that are supplying the wart with nutrients and oxygen.

Can Warts Be Prevented?

Though skin warts can’t be prevented, there are a number of precautionary measures you can take to minimize your risk of acquiring warts. One of the most important things you can do is to wash your hands regularly. Also, try to keep your skin healthy, moisturized, and free of cuts. If you bite your fingernails or cuticles, do your best to stop. Biting nails creates an opening for virus to enter your skin. Be careful to use clean, fresh towels at the gym or in other public locations, and always wear rubber-soled flip-flops or sandals in public locker rooms and showers.

Will Warts Go Away On Their Own?

Some warts will go away without treatment, others will not. Even those warts that eventually go away can take months, or even years, to disappear. Also, keep in mind that any wart can be a “mother” wart that spreads to other parts of your body. Most dermatologists say it is best to treat warts, either at home or in the doctor’s office, as soon as they appear.

Monday, May 12, 2014

"UKAWA INAANZA TANZANIA BARA": RATIBA YA ZIARA YA AWAMU YA KWANZA YA UKAWA, TAREHE 14 – 27 MEI 2014.

"UKAWA INAANZA TANZANIA BARA"
RATIBA YA ZIARA YA AWAMU YA KWANZA YA UKAWA,
TAREHE 14 – 27 MEI 2014.
TIMU “A”- KANDA YA KATI
1. Mhe. Mosena Nyambabe (NCCR) – Katibu Mkuu,
2. Mhe. Ashura Mustapha (CUF) – Mjumbe wa Baraza Kuu,
3. John Heche (CHADEMA) – Mwenyekiti wa Vijana Taifa,
14/05/2014 MOROGORO MJINI
16/05/2014 SHINYANGA MJINI
17/05/2014 BARIADI MJINI
18/05/2014 NZEGA MJINI
19/05/2014 TABORA MJINI
20/05/2014 URAMBO
22/05/2014 NGURUKA
23/05/2014 KIGOMA MJINI
24/05/2014 MNANILA
25/05/2014 KASULU MJINI
26/05/2014 KASULU VIJIJINI
27/05/2014 KIBONDO MJINI
TIMU “B” – KANDA YA KASKAZINI
1. Dr Willibroad Slaa(CHADEMA) – Katibu Mkuu,
2. Mhe. Mustapha Wandwi (CUF) – Mjumbe wa Baraza Kuu,
3. Ahmed Msabaha (NCCR) – Mjumbe wa Halmashauri Kuu,
TAREHE ENEO LA MKUTANO
14/05/2014 MOSHI MJINI
15/05/2014 BABATI MJINI
16/05/2014 ARUSHA MJINI
18/05/2014 MUSOMA MJINI
19/05/2014 TARIME MJINI
20/05/2014 BUNDA MJINI
21/05/2014 BIHARAMULO MJINI
22/05/2014 BUKOBA MJINI
23/05/2014 KARAGWE MJINI
24/05/2014 NGARA MJINI
25/05/2014 KATORO
26/05/2014 GEITA MJINI
TIMU “C” – NYANDA ZA JUU KUSINI
1. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba(CUF) – Mwenyekiti,
2. Mhe. Said Issa (CHADEMA) – Makamu Mwenyekiti Taifa,
3. Martin Juju Danda(NCCR) – Mjumbe wa Halmashauri Kuu,

TUNAPASWA KUFUNGA MILANGO YA UCHOCHORO KIGOMA ILI KUNUSURU WIZI NA UBADHILIVU UNAORUDISHA NYUMA KIGOMA


By Butije H. 
"Fedha za miradi ya maendeleo Tsh 10,000. Fedha za matumizi ya kawaida Tsh 100,000" Kwa bajeti hii ya kutengwa kwa kiwango kikubwa cha fedha kwenye matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kutengewa fedha kiduchu hatutafika.
Ajabu ya kuogofya hapa ni kuengwa kwa bajeti halafu fedha inayopelekwa na serikali haifiki hata 50% ya fedha iliyotengwa na ile iliyopelekwa kutumika zaidi ktk matumizi ya kawaida na si miradi ya maendeleo.
Miaka kadhaa halmashauri nyingi zimekuwa zikipata hati chafu baada ya ukaguzi CAG lakini hakuna hatua za kinidhamu wala kisheria zinazochukuliwa kwa walihusika na kuchafua halmashauri hizo.
Nchi hii inaliwa na watawala tunahitaji kuwa na viongozi. Kila mwaka ambao wananchi wanapata fursa ya kuchagua viongozi wanajikuta wanapewa kitu kidogo na watawala na hatimae kuwarejesha watawala madarakani.
Msiba mkubwa ni pale anapokuja mtawala na sura iliyo na bashasha na sura ya kinafiki ya kukujali sana anakwambia naomba kura yako laikini chukua na hii (BUKU) itakusaidia kwa leo. Then hakuna zahanati anayojenga halafu mke wako anapotaka kujifungua zahanati inapatikana mbali unaomba mchango (20,000) kwa rafiki zako ukodi TAX umpeleke mkeo kituo cha afya kilichopo mbali ukajifungue.
Utamsikia mtawala huyo anakwambia ukinichagua nitashughulika nihakikisha shule ya chekechea hapa mtaani inakuwa na madawati lakini chukua hii (BUKU) itakusaidia leo. Anatoa buku hizo kwa watu zaidi na zaidi na zaidi fedha ambazo angeweza kununua madawati ya kutosheleza shule zaidi 100.
Hivi kweli huyu mzee wa BUKU analengo la kutatua tatizo la madawati au analengo la kutufanya tuendelee kukaa chini na kukosa ari ya masomo ili tufeli nae aendelee kututawala badala ya kutongoza?
Mwaka 2005 & 2010 neno BUKU, BUKU MBILI, BUKU TANO na HATA BUKU ZAIDI ilikuwa ndio wimbo wa njini huku ahadi lukuki zikitolewa na moja ya hadi hiyo ni kumaliza tatizo ln "NITAHAKIKISHA MABOMBA YOTE YANATOA MAJI, NAJUA SHIDA NA ADHA MUIPATAYO WANANCHI WA KIGOMA, SASA NASEMA SASA BASI, NATAMBUA TUNAKOSA MAJI BILA SABABU YOYOTE WAKATI TUNAZIWA TANGANYIKA AMBALO TUNAWEZ KUPELEKA MAJI YA BOMBA HATA TABORA"
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 nilipata faraja kuwa huwenda tatizo la maji likawa historia ndani ya manispaa ya Kigoma/Ujiji nikiamni kuwa tunawapinzani wanaotetea maslahi ya wananchi na tunawatawala wanaotaka kuonesha kuwa wao sio watawala bali ni viongozi wanaosikiliza kilio cha wananchi.
Mbunge wa CCM ambae anatoka katika chama chenye dola atahakikisha udola na mamlaka walonayo wanamaliza ukame na kutu zinazoendelea kutafuna mabomba yetu ambayo kutu hizo zinaweza kutusababishia maradhi mbalimbali kwa miaka michache ijayo kwa kutumia maji ambayo yanapatikana kama ngekewa.
Kwa upande mwingine halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeshikwa na upinzani huku wakijivunia kwa kuwa na meya kijana lakini nao wameshindwa kutatua adha wanayoipata mama, dada, kaka na ndugu zetu wote walioko Kigoma.
Hivi kigoma kunanini? Hapa mchawi anaeturoga tusiendelee ni nani? Ni wazi kuwa rasilimali na utajiri ulioko mkoani kwetu ndo mchawi wetu. Mwabwanyenye wanaharibu na kufunga kila mlango wa mpango wa kuendeleza mkoa wa Kigoma. ili wafungue mlango wa uchochoro na kutorosha na kutumia rasilimali za kigoma kwa maslahi yao.
Hao mabwanyenye wanajaribu hata kuandaa watawala na si viongozi ili wakatetee na kuendelea kufungua milango ya uchochoroni kwa maslahi yao binafsi.
Hivyo BACK TO KIGOMA MOVEMENT ni muhimu ili kwenda kufunga milango yote ya uchochoroni ili kufungua milango ya barabarani ambayo itakuwa na tija na neema kwa wanakigoma wote.
Wakazi wa KIGOMA vijana wenu wanaona uonevu katika mkoa wetu basi. Ni wakati wa kurejesha hadhi ya mkoa wetu.
Mungu ibariki LWAMA
Mungu wabariki WANALWAMA

Sunday, May 11, 2014

Man City seal Premier League title

Manchester City won a second Premier League title in three years as goals from Samir Nasri and captain Vincent Kompany secured victory over West Ham
The Sky Blues, needing a draw to guarantee being English champions for the fourth time, dominated before Nasri fired in off the post from 20 yards.
David Silva hit the bar before half-time, but Kompany prodded in from six yards to seal a fifth win in a row.
City finished two points ahead of Liverpool, who beat Newcastle 2-1.
The Reds' victory was academic as City eased past Sam Allardyce's side, reaching 102 league goals for the season, one shy of Chelsea's record in 2009-10

JULIUS S. MTATIRO: VYAMA VIPYA VYA SIASA VINAWEZA KUWA NA MAANA KUBWA NA VINAWEZA KUWA HOVYO MNO

ALLAH Ibariki Nchi Yetu

VYAMA VIPYA VYA SIASA - MTIZAMO BINAFSI.
Vyama vipya vya siasa vinavyoanzishwa na kusajiliwa nchini Tanzania vinaweza kuwa na maana kubwa sana, na vinaweza kuwa hovyo mno.
Tayari tunajua kuna chama kikubwa hapa nchini na kinatumia kila mbinu NZURI na CHAFU kuendelea kuongoza nchi. Na kuna vyama vya upinzani vyenye ushawishi mkubwa lakin kutokana na sababu mbalimbali vyama hivyo havijaweza kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi kwa miaka 20 sasa.
Vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR vina ushawishi mkubwa sana hivi sasa, kila kimoja kikiwa na maeneo kadhaa makubwa ambayo kinaweza kushinda ikiwa vyama vingine vitakiunga mkono.
CCM imeendelea kushikilia maeneo makubwa zaidi na kushinda chaguzi mbalimbali kwa kutumia nafasi ya;
(1) kuwa na tume ya uchaguzi inayoteuliwa na CCM haohao,
(2) kuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha unaochota fedha kutoka serikalini, miradi ya chama ambayo wananchi waliporwa na kufanywa ya CCM, matajiri wengi wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kupata upendeleo wa shughuli zao, mataifa makubwa duniani yanayonufaika na mfumo wa CCM kuendelea kuwepo madarakani n.k.

Saturday, May 10, 2014

KIFO CHA SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU NI MSIBA KWA VIJANA- MOHAMED SAID

Written By Mohamed Said

Sheikh Ilunga Hassa Kapungu 1988

Aliyekaa Katikati ni Ilunga Hassan Kapungu na Kushoto Kwake
ni Ali Salum Mkangwa na Aliyesimama Nyuma ni Mwandishi
Nyuma  Wapili Bakari Saleh Mwisho Kulia Ilunga  Hassan Kapungu
Mstari wa Mbele Watatu Kutoka Kushoto Mwandishi
Hawa ni Baadhi ya Vijana wa Kiislam Waliohudhuria Semina Dodoma
Chuo Cha Biashara 1988
Sheikh Ilunga Hassan Kapungu kaingia katika historia ya Dar es Salaam katika kifo chake. Bahari ya watu waliojazana Msikiti wa Kichangani kuja kuswalia jeneza lake na kisha kulifata nyuma jeneza hilo hadi Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Mapipa haijapatapo kuonekana. Sheikh Ilunga ni ''mgeni'' katika mji wa Dar es Salaam kwa maana ya kuwa hakuzaliwa Dar es Salaam wala hakuwahi kuishi Dar es Salaam wala hakuweza kujinasibu kwa lolote au chochote katika mji wa Dar es Salaam. Alikuwa akija na kuondoka zamani akirejea kwao Tabora na baadae baada ya kuhamia Mwanza, akija Dar es Salaam na kurejea Mwanza. Iweje leo mji mzima wa Dar es Salaam usimame na utoke kuja kumzika Sheikh Ilunga Hassan Kapungu? Hakika hili ni swali linalotaka majibu ya kuridhisha. Jibu ni dogo na rahisi sana. Hivi ndivyo Waislam wanavyofanya dunia nzima kila wanapofiwa na kipenzi chao. Labda linaweza kuja swali jingine, ''kipenzi?'' Sheikh Ilunga kawaje kuwa kipenzi cha Waislam? Naam Sheikh Ilunga Hassan Kapungu juu ya udogo wake wa umri alikuwa kipenzi cha Waislam na si Waislam wa Dar es Salaam peke yao. Sheikh Ilunga alikuwa kipenzi cha Waislam wa Tanzania nzima. Kibla cha kila msikiti wa Waislam katika Tanzania kilikuwa kinamkaribisha kama si kuwaidhi basi angalau asimame awasalimie nduguze Waislam. Sheikh Ilunga alipendwa na umma hakuwa katika lile kundi la mesheikh wanaoogopa kuswali katika baadhi ya misikiti au hata kupita nje yake. Sheikh Ilunga hakuwa katika lile kundi la masheikh wenyeji katika futari za serikali na''misikiti ya wakubwa'' lakini wageni katika misikiti ya ndugu zao Waislam, Manzese au Tandale. Kubwa Sheikh Ilunga hakukosa usingizi wala kujiona duni kwa kukosa kualikwa futari Ikulu au kualikwa katika dhifa za kitaifa akapigwa picha kavaa kanzu za kupendeza kakaa na waheshimiwa na kutokea katika runinga na magazeti siku ya pili ukurasa wa mbele. Sheikh Ilunga Hassan Kapungu hakushughuliswa na hayo. Yeye alishughulishwa na kuliweka juu jina la Allah Subhana Wataala. Hili ndilo lililokuwa likimshughulisha mpaka siku Allah alipomuhitimisha.

Sheikh Ilunga kaweka historia katika historia ya mazishi makubwa Dar es Salaam, historia inayokwenda nyuma kiasi miaka takriban 100 ukianzia mazishi ya Sheikh Mwinyikheri Akida sheikh aliyeasisi Msikiti wa Mwinyikheri Akida Kisutu, unakuja kwa Sheikh Idrissa bin Saad Khalifa wa Tariqa Askariyya, kisha Sheikh Kaluta Amri Abeid, halafu Abdulwahid Sykes, kisha Sheikh Kassim bin Juma, halafu Sheikh Abbas Kilima. unakwenda kwa Prof. Kighoma Ali Malima unaishia kwenye maziko ya Mzee Kitwana Dau baba yake Dk. Ramadhani Dau. Iweje Ilunga kijana mdogo mno aungane na majina ya watu maarufu kama hawa na kupata maziko makubwa kiasi kile? Kitu kilichompandisha daraja Ilunga katika umma wa Waislam Tanzania ni kuwa Ilunga alikuwa mtumishi wa Waislam. Wakimtuma Ilunga kila kazi na akiifanya kwa moyo mkunjufu, kuanzia kujenga madras na shule hadi kuwasomeshea watoto wao. Juu ya haya yote kilele cha Sheikh Ilunga katika kuutumikia Uislam ni ile siku aliposimama Ukumbi wa Diamond kuitahadharisha serikali kuwa kuna ''Mfumokrsisto'' nchini unaotawala na kudhulumu haki za Waislam. Hii ilikuwa mwaka 2012. Nilikuwa mmojawapo wa Waislam waliokuwa pale ukumbini kushuhudia kitendo kile cha kihistoria. Kwa nini nakiita kitendo cha kihistoria? Nakiita kitendo cha kihistoria kwa kuwa kwa takriban miaka 40 Waislam walikuwa wanasemea pembeni harakati zikienda chini kwa chini vijana wakiwatayarisha Waislam wajue kuwa ipo dhulma.

Sheikh Hussein Malik alikuwa akisema, ''Wafahamisheni Waislam wajue kuwa ipo dhulma kisha wadaie haki zao. Ikiwa utawadaia haki zao ikiwa hawajui dhulma ipo, wao ndiyo watakuwa wa kwanza kukupigeni vita kwani kama mtu hajui anadhulumiwa basi hiyo dhulma haipo.'' Sheikh Ilunga alikuwa katika kundi la vijana waliokuwa wakihangaika kuitafuta haki ya Waislam. Siku ile pale Ukumbi wa Diamond wakati ulikuwa umefika na kwa niaba ya Waislam Sheikh Ilunga akasimama kuitahadharisha serikali kuhusu kuiachia dini moja ikahodhi fursa zote za nchi kwa hila. Hotuba ya Sheikh Ilunga ilirushwa na Radio Imaan na TV yake mubashara, yaani ''live.'' Kote Radio Imaan ilikosikika Waislam walimsikia Sheikh Ilunga akieleza nini Waislam walifanya katika Tanganyika wakati wa kupigania uhuru kuuondoa dhulma na kuleta haki kwa kila mwananchi na vipi Waislam walisalitiwa baada ya uhuru kupatikana. Vyombo vyote vya habari ukitoa vile vya Kiislam viligoma kabisa kutangaza kongamano hili la Waislam. Ikawa kama vile hapajapatapo kutokea kitu chochote. Waislam hawakukata tamaa kuanzia siku ile Sheikh Ilunga alitembea nchi nzima na kufanya mikutano ya hadhara kuitahadharisha kwanza serikali kuhusu Mfumokristo na pili Waislam wa Tanzania khasa wale waliokuwa gizani ili wajue nini kilikuwa kinawatafuna.

Msikiti Umejaa Hadi Nje

Prof. Ibrahim Lipumba Akiswali Nje ya Msikiti kwa Kukosa Nafasi Ndani

Gari ya Maalim Seif Ikitoka Msikiti wa Kichangani
Kuelekea Makaburi ya Mwinyimkuu
Jeneza la Sheikh Ilunga Likitolewa Msikitini
Nilimfahamu vipi Sheikh Ilunga Hassan Kapungu? Nilianza kuzisikia sifa zake katika miaka ya 1980 kabla sijauona uso wake. Wakati ule Sheikh Ilunga alikuwa kijana mdogo sana na mdogo kwangu kwa miaka kadhaa. Wakati naingia kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Ilunga alikuwa maarufu pale chuoni msikiti wa Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) kiasi unaweza ukadhani kuwa na yeye ni mwanafunzi. Ilikuwa Ilunga na wenzake akina Mohamed Kassim Lulengelule ndiyo walioleta ''Nyaraka za Waikela'' na kuzihifadhi katika maktaba ya MSAUD. Hizi nyaraka zilikuwa zimefichwa Tabora kwa karibu miaka 20. Katika nyaraka hizi kulikuwa na kisa kizima cha kile kilichokuja kujulikana kama ''Mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS),'' Ndani ya jalada zilimohifadhiwa nyaraka zililofikishwa MSAUD kulikuwa na kumbukumbu za mikutano ya EAMWS, taarifa ya Kamati ya Upatanishi iliyokuwa inajaribu kupatanisha kati ya kundi la Adam Nasibu na wenzake waliokuwa wanampiga vita Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Patron wa  EAMWS Aga Khan na Katibu wa jumuia hiyo Tanzania, Aziz Khaki; kulikuwa na ''cuttings'' ya magazeti ya ''Uhuru,'' ''Nationalists'' na ''Tanganyika Standard,'' magazeti makubwa ya zama zile yaliyokuwa yakifuatilia kwa karibu sana mgogoro ule. Ndani ya jalada lile kulikuwa na taharir ya ''The Nationalist,'' ambalo Mhariri Mkuu wake alikuwa Benjamin William Mkapa na pia kulikuwa na tahariri ya ''Tanganyika Standard,'' ambalo Mhariri Mkuu alikuwa Brendan Grimshaw. Tofauti ya tahariri hizi ni kuwa wakati tahariri ya Mkapa ilikuwa ikishambulia uongozi wa EAMWS tahariri ya Grimshaw ilikuwa ikiomba sulhu ipatikane. Nyaraka hizi za Mzee Bilal Rehani Waikela zilikuwa hazina kubwa. Kutokana na nyaraka hizi ndipo ukweli wa nini na nani alikuwa nyuma ya kuvunjwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA ukafahamika. Lakini kubwa zaidi waliokabidhiwa Nyaraka za Waikela walizileta zikiwa na maelezo ili maelezo yale yaende na kile kitakachosomwa ndani ya jalada. Ilikuwa wazi kuwa hapakuwa na mgogoro katika EAMWS. Kilichofanya Nyerere aipige marufuku EAMWS na kumfukuza Sheikh Hassan bin Amir Tanganyika kumrudisha Zanzibar ni kuwa Kanisa Katoliki halikupenda Waislam wajenge Chuo Kikuu na tayari jiwe la msingi lilikwishawekwa na yeye mwenyewe Nyerere. Katika maelezo yake Mzee Waikela aliweka na majina ya Waislam wanafik walioipiga vita EAMWS.

Hii Picha Ilipigwa Siku ya Julius Nyerere Alipoweka Jiwe la Msingi
Chuo Kikuu Cha Waislam, Chang'mbe 1968 Nyerere 
Anapeana Mkono na Mufti Sheikh Hassan bin Amir Katikati yao
ni Tewa Said Tewa Rais wa EAMWS Tawi la Tanganyika
Ilunga alikuwa kijana wa Mzee Waikela. Katika hali ya unyonge sana walikuwa wakiendesha shule ya Nujum katika juhudi za Waislam kujitoa katika dhulma ya elimu. Mzee Waikela alimsomesha vyema Ilunga kuhusu fitna na chuki ya Nyerere kwa Uislam na Waislam na mbinu zinazotumika kuudhalilisha Uislam. Bilali Rehani Waikela alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU Western Province mwaka wa 1955 na ni yeye na wazee wake akina Abdallah na Maulidi Kivuruga na wazalendo wengine ndiyo waliomleta Nyerere Nyerere na Bi. Titi Mohamed kuja kuitia nguvu TANU Tabora. Ilunga akasomeshwa na Mzee Waikela historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na akaijua na yeye maisha yake yote akaisomesha kwa wanafunzi wake. Mzee Waikela vilevile alikuwa Katibu wa EAMWS Western Province. Mzee Waikela alikuwa mfano na kigezo kikubwa kwa Ilunga katika maisha yake ya kuwatumikia Waislam na kwa upande wake Ilunga alikuwa mwanafunzi hodari na aliteka ilm nyingi kwa huyu mwalimu wake.

Nyaraka za Waikela hizi nilizikuta Maktaba ya MSAUD na nilisoma jalada lile tena na tena. Wakati nazisoma nyaraka zile nilijihisi kama Edward Crankshaw siku alipofikishiwa mswada wa kitabu cha Nikita Kruschev ''Kruschev Remembers,'' mswada uliovushwa kwa siri kutoka Urusi hadi Amerika kutafuta ''publisher.''  Kwangu mimi ilikuwa kweli nasoma yaliyokuwa ndani ya jalada lakini hapo hapo akili yangu inakataa kuamini kuwa kweli hii ndiyo kweli yenyewe.  Nikaweka azma ya In Sha Allah kwenda Tabora kuonana na na Ilunga na Mzee Waikela. Hivi ndivyo nilivyokutana na Sheikh Ilunga kwa mara ya kwanza mwaka 1987 na yeye na shemeji yake Salum Ali Mkangwa wakanipeleka kwa Mzee Waikela. Msomaji zingatia kuwa haya yote ambayo Ilunga aliyokuwa akisomeshwa na Mzee Waikela kuhusu hujuma dhidi ya Uislam ilikuwa kabla hata John Sivalon hajaandika kile kitabu chake maarufu, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985 (Ndanda, 1992). Kitabu hiki ni maarufu kwa Waislam hakihitaji maelezo.

Mzee Bilali Rehani Waikela Amesimama Mbele
ya Mahakama ya Kisutu Alikokuja Kutoa Ushahidi Katika
Kesi ya Sheikh Issa Ponda Kuhusu Mali za EAMWS

Julius Nyerere na Bi. Titi Mohamed Katika Miaka ya 1950 Wakati
wa Kupigania Uhuru wa Tanganyika

Sheikh Hamid Jongo

Turudi nyuma kidogo. Baada ya kuonana na Ilunga Tabora mwaka 1987 tukajakuonana tena mwaka 1988 katika semina ya vijana wa Kiislam ''Unity of Muslim Umma'' iliyowakusanya vijana wa Tanzania Bara na Visiwani iliyofanyika Dodoma. Mmoja katika wahadhir katika semina ile alikuwa Sheikh Hamid Jongo ndiyo kwanza anatokea masomoni Saudi Arabia. Alikuwapo pia Sheikh Mangocho (sasa ni Sheikh wa BAKWATA Mtwara).Wakati ule sote tulikuwa bado vijana na sote tukipambana na BAKWATA. Katika semina hii alikuwapo marehemu Mussa Mdidi, Waziri Nyelo, Salum Abdallah Amour, Faiz Iddi Faiz Mafongo, Abdulkadir Faya, Ahmed Olotu, Said Kambi, Ahmed Omar Mnyanga, Sheikh Hassan Mnjeja, Sheikh Hussein Abdallah wa Tanga, Sheikh Ali Kilima katika wachache ninaowakumbuka. Nakumbuka mada aliyotoa Sheikh Ali Kilima ambayo ilijaa changamoto kwa vijana wasomi wa Kiislam wa enzi zile. Mada yake ilikuwa inauliza: ''Mlango wa Kujitahidi Umefungwa?'' Sikushangaa miaka mingi baadae kujamuona Sheikh Ali Kilima sasa si kijana tena bali ni mtu mzima akijishughulisha na tafasiri na uchapaji wa vitabu vya Kiislam. Dalili zilikuwapo toka siku za mwanzo. Semina hii kwetu sote ilikuwa kama semina ya kuuaga ujana kwani wengi wetu  tulikuwa tukielekea katika utu uzima na wengi kati yetu wametangulia mbele ya haki.

Kushoto Kwenda Kulia: Faiz Iddi Faiz Mafongo na Mussa Mdidi

Kushoto Kwenda Kulia: Salum Abdallah Amour (Zanzibar),
Sheikh Hussein Abdallah (Tanga) na Sheikh Ali Kilima (Dar es Salaam)

Ilikuwa katika semina hii ndipo kwa mara ya kwanza nilipofahamiana na Sheikh Issa Ponda. Ninachokumbuka kwa Sheikh Ponda ni kuwa alitusalisha sala moja na niliusikia usomaji wake mzuri wa Qur'an. Nilimpenda kutoka siku hiyo. Semina hii ilikuja baada ya mambo mengi dhidi ya Uislam kutokea nchini. Kulikuwa na sakata la Sophia Kawawa kutaka Qur'an ibadilishwe. Hii ilitokea mwezi Mei 1988. Baada ya kauli hiyo palifanyika maandamano makubwa Zanzibar kumpinga Sophia Kawawa na Waislam walishambuliwa, baadhi wakauliwa na wengine wakapata ulemavu wa maisha. Sheikh Said Gwiji mshtakiwa namba moja na wenzake walishitakiwa na wakafungwa jela miezi 18. Kosa lao likiwa ni kuihami Qur'an ya Allah isichezewe. Kulikuwa na vita vikipigwa dhidi ya vazi la hijab na kesi maarufu ilikuwa ya Fikira Omari mfanyakazi wa Kiltex. Kulikuwa na kesi ya Kurwa Shauri  aliyeshitakiwa kwa ''uchochezi'' na mambo mengine. Katika hayo kulikuwa na tatizo la Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akimbughudhi Rais Mwinyi na kuwashambulia Waislam hasa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu. Kulikuwa na pia na ''Christian Lobby,'' mtandao wa siri katika vyombo vya habari vilivyokuwa vikiwapiga vita Waislam waliokuwa katika serikali ya Rais Mwinyi achilia mbali kuupiga vita Uislam wenyewe wakitumia nafasi zao katika vyombo hivyo.

Aliyesimama Mchungaji Christopher Mtikila
Kipindi hiki kilikuwa kigumu sana kwa Waislam khasa kwa kuwa rais aliyekuwa madarakani alikuwa Muislam, Ali Hassan Mwinyi. Kubwa zaidi ni kuwa Nyerere aliwaacha Waislam katika hali mbaya sana ya unyonge kwa kuitumia BAKWATA. Vijana wa Kiislam kupitia WARSHA walikuwa na mtandao wa aina yake wakifuatilia kila jambo na kujitahidi kuuhami Uislam. Sheikh Ilunga hakuwa mchezea pembeni, alikuwa katikati ya harakati hizi zote. Semina hii ilipokuja ilitukutanisha wengi tukajuana kwa sura na majina. Uelewa wa Ilunga katika harakati hizi ulijitokeza wazi katika semina ile. Baada ya sala ya Alfajir katika semina ile Ilunga alikimbilia uwanja wa mpira wa kikapu kupiga ''shots'' katika kikapu. Ndipo nilipokujakujua kuwa Ilunga alikuwa mchezaji bingwa wa mchezo huu. Nilistaajabu sana kuona jinsi alivyokuwa mwepesi kuruka na kukimbia achilia mbali kuwa na umbo kubwa. Baadhi yetu katika kundi hili halikufika mwisho wa safari. Walishuka njiani na kupanda treni nyingine iliyokuwa inaelekea upande mwingine na ndiyo maana leo wamekuwa masheikh na ''makadhi'' wa BAKWATA.


Sheikh Said  Suleiman Masoud (Gwiji) Kama Alivyo Hivi Sasa
Picha Hii ni Katika Hafla ya Uzinduzi wa Muslim
Development Fund (MDF) Ukumbi wa Diamond 2004

Sheikh Gwiji Akifanya Mahojiano ya TV na Mwandishi Nyumbani Kwake
Zanzibar Mwaka  2012 Akimweleza Mitihani Waliyopitia Katika Kadhia ya
 Sophia Kawawa  Baada ya Kuhukumiwa Kifungo Cha Miezi 18
Vijana wa Kizanzibari Waliohukumiwa Kwenda Jela Kwa Kuihami Qur'an
Wakisindikizwa Baada ya Kuhukumiwa Kifungo Waliingia Jela kwa Furaha
ya Kupata Sunna ya Nabii Yusuf na Kusadikisha Yale Allah Aliyoahidi

Miaka ya 1990 Sheikh Ilunga alikuwa amehamia Mwanza akitokea Tabora. Hii ilikuwa baraka kubwa kwa Mwanza kwani mara tu alipofika alianza kuendesha darsa katika misikiti na kutoa mihadhara. Alianza kufundisha somo la Maarifa ya Kiislam katika shule mbalimbali na akaweka darsa la kudumu Msikiti wa Sheikh Alamin Maftah mbali na kuendesha darsa duara kadhaa. Hapo ndipo yeye na wenzake wakaamua kujenga shule - Nyasaka Islamic Secondary. Haikupita muda hali ya Mwanza ikabadilika darsa za Sheikh Ilunga zilizaa matunda vijana walijitathmini upya na taratibu umoja wa Kiislam ukaimarika na hii iliingia hadi BAKWATA. Viongozi waliochaguliwa kuongoza BAKWATA walikuwa kweli viongozi na viongozi hawa wakawa sasa wanafanya kazi ya Allah. BAKWATA ya Mwanza ikawa tofauti na BAKWATA nyingine nchini. Kuna siku Ilunga alinifahamisha kuwa BAKWATA ya Mwanza inamtumikia Allah, Waislam wasiwe na hofu yoyote. Alinifahamisha kuwa msimamo waliouweka ni kutiana nguvu katika yale ambayo wanakubaliana, mathalan elimu kwa vijana. Haukupita muda mrefu Mwanza ukawa mji wa kupigiwa mfano katika juhudi za maendeleo ya Waislam na Ilunga alikuwa katikati ya juhudi hizi. Ilikuwa katika kipindi hiki siku moja usiku wa manane Ilunga akavamiwa nyumbani kwake na ''majambazi.'' Haya ''majambazi,'' yalikuwa matatu. Mmoja alibaki nje akilinda doria na wawili walivunja mlango na kumwingilia ndani na mapanga. Ilunga nilivyokwishaeleza alikuwa mtu wa miraba minne. Alikabiliana nao na nyasi zilisagika hata hivyo Ilunga aliumizwa vibaya sana. Wakati yale majambazi yanakimbia kutoka ndani Ilunga alimsikia mmoja akimuuliza mwenzake, ''Vipi umemmaliza?'' Jibu likatoka, ''Utasikia kesho.'' Nilipokuja kukutana na Ilunga nilimuuliza ni nani waliotaka kumuua. Ilunga alinifahamisha. Akasema ''Wale niliopigananao wote wawili walikuwa wamevaa buti zilizofanana na buti hizo nazijua zinapovaliwa lakini sina ushahidi zaidi ila Allah ndiye mjuzi.''


Sheikh Issa Ponda

Mauaji ya Waislam Msikiti wa Mwembechai mwaka 1998 lilikuwa jambo kubwa katika historia ya Uislam. Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu mauaji yale Waislam walimualika Sheikh Ilunga aje azungumze Msikiti wa Mtambani. Kipindi hiki Sheikh Ponda alikuwa amejificha baada ya kupata taarifa kuwa anataka kukamatwa. Waislam walikuwa na ghadhabu na serikali ya Mkapa. Hali ilikuwa ya wasiwasi sana. Dar es Salaam ilikuwa haijamsikia Ilunga. Siku ile ndipo walipokiona kipaji chake cha kuzungumza. Hadhira ile ilikuwa kama vile imemwagiwa maji baridi. Sauti iliyosikika ikiunguruma katika vipaza sauti vyenye nguvu kubwa vya Mtambani ilikuwa sauti ya Ilunga ikipokewa hapa na pale za vibwagizo vya ''Takbir Allahu Akbar.'' Kamera zilizokuwa mbele ya kibla kuchukua tukio lile zilikuwa hazihesabiki. Video za Sheikh Ilunga zikasambazwa nchi nzima na athari yake ilikuwa kubwa sana. Wale Waislam walikuwa hawajui kinachotendeka nchini walianza kujua ukweli wa mambo. Kilio cha Waislam kuhusu dhulma kikawa sasa kinatambaa nchi nzima. Serikali nayo kwa upande wake ilizidi kuwaandama masheikh na viongozi wa Waislam na hii ikapelekea kuzinduliwa Azimio la Tungi. Hakuna aliyeshangaa siku viongozi wa Waislam walipokusanyika Msikti wa Tungi na kutoa ''Azimio la Tungi,'' ambako kwa mara ya kwanza neno ''Mfumokristo'' lilitumika. Msomaji wa Azimio la Tungi alikuwa Sheikh Ilunga Hassan Kapungu. Azimio la Tungi lilikuwa Azimio la vita. Vyombo vyote vya habari havikuweza kuandika Azimio la Tungi limesema nini. Maneno yaliyokuwa ndani ya Azimio lile yalikuwa maneno mazito yenye ukakasi uliokusudiwa. Ilikuwa baada ya Azimio la Tungi ndipo Waislam baada ya matayarisho ya kutosha wakasimama Ukumbi wa Diamond kuieleza serikali kuwa inaendeshwa na Mfumokristo. Yaliyobaki ni historia. Unahitaji kuandika kitabu kizima kumweleza Ilunga. Ilunga alikuwa jasiri  mtu asiye na uoga wa kumuogopa yeyote yule. Sheikh Ilunga amesomesha vijana wengi sana katika maisha yake na bila ya yeye mwenyewe kusema kwa dhahiri. Ukiangalia maisha yake na kama ulibahatika kuhudhuria darsa zale utajua kuwa Sheikh Ilunga alikuwa anawalenga vijana na kwa hakika niliwaona vijana wake wengi katika maziko yake.

Kwa kuhitimisha turejee nyuma zaidi na kuangalia wapi historia hii imetoka hadi kufikia Sheikh Ilunga. Hebu tujiulize vipi mahali kama Tabora juu ya hali ilivyokuwa ngumu imeweza kumtoa mtu kama Sheikh Ilunga? Kupata jibu inakubidi uwatazame wale waliomlea Ilunga. Uitazame silsila ya Ilunga kuanzia kwa mzee na mwalimu wake, Mzee Waikela, kisha umtazame na yeye mwenyewe Mzee Waikela na wale aliokuwanao katika kuutumikia Uislam katika miaka ya 1950 wakati wa ukoloni. Huwezi kumtaja Sheikh Ilunga katika kuupigania Uislam ukaacha kutamtaja Mzee Waikela. Huwezi kumtaja Mzee Waikela usimtaje Sheikh Hassan bin Amir. Sheikh Ilunga kaingia katika mnyororo ya silsila ya watu hawa. Hao watakaokuja baadae wataisoma historia hii na silsila hii na kila wakiwarehemu waja hawa wema Sheikh Ilunga atatajwa pia kwa wema pamoja nao. Nani hii leo katika sisi asiyetaka kunasibishwa na historia iliyoachwa na watu hawa? Historia inayoanza miaka ya 1940 na Sheikh Hassan bin Amir akizunguka Tanganyika nzima hadi Congo, Malawi., Rwanda na Burundi kueneza Uislam. Inapokelewa na Mzee Waikela katika miaka ya 1950 wakati wa kudai uhuru akiwa mmoja wa vijana wa Sheikh Hassan bin Amir na mkono wa kulia wa sheikh. Harakati hizi zinakuja kupokelewa na kijana wa baada ya uhuru, Ilunga Hassan Kapungu katika miaka ya 1970 mwishoni. Hakika historia hii ni ya kuandikwa kwa wino wa dhahabu. Sheikh Ilunga kama wale waliomtangulia walivyofanya, wale waliomfanyia Allah na Mtume wake SAW uadui yeye hakuwafanya marafiki zake. Hadi umauti unamfika Sheikh Ilunga alikuwa anakabiliwa na kesi ya ''uchochezi'' na video zake zinatafutwa na vyombo vya dola. ''Uchochezi '' uliokusudiwa na hao waliomfikisha mahakamani ni kwa Sheikh Ilunga kuidai haki ya Waislam iliyoporwa. Hakika Waislam tumepoteza jemadari.

Wanne Kutoka Kushoto Aliyevaa Kofia ni Sheikh
Chambuso
Baada ya maziko nilimuona mmoja wa vijana wake Sheikh Chambuso Rajab Ramadhani kutoka Tanga na wenzake wamelibeba jeneza lililombeba mwalimu wao wanalirudisha msikitini wakiwa katika majonzi mazito.

Allah amsamehe ndugu yetu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu makosa yake na amjazie pale palipopungua na amtie katika Pepo ya Firdaus.
Amin.

BUTIJE NA MOHAMMED SAID NDANI YA STUDIO ZA RADIO KHERI DAR ES SALAM


Saturday, May 3, 2014

MIVITANO YAANZA NDANI YA UKAWA

WAKATI viongozi wa kile kinachoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanaonesha kushikamana hadharani, habari za ndani ya Umoja huo zinasema kuwa mivutano imeanza kuzuka huku baadhi ya viongozi wake wakitaka kurejea Bunge Maalum la Katiba.

Habari kutoka ndani ya Umoja huo zinasema kuwa angalau viongozi wawili wa vyama vinavyounda UKAWA wanataka kurejea bungeni na kushiriki mchakato wa kutunga Katiba mpya wakati Bunge hilo litakapoanza tena Agosti mwaka huu.

Habari zinasema kuwa viongozi hao wawili, wanataka kurejea tena bungeni kwa sababu wameanza kubaini kuwa kuna ujanja mwingi ndani ya UKAWA na kuwa baadhi ya vyama vinavidanganya na kuvitumia vingine, bila kuonekana kwa faida yoyote dhahiri.

“Tulisusa Bunge kwa pamoja, lakini sasa inaanza kuonekana kuwa wapo wenzetu ambao wana maslahi binafsi na kuonekana kututumia sisi kwa manufaa yao ya kisiasa na hata kifedha,” anasema mmoja wa viongozi wa UKAWA, ambaye anahisi baadhi ya wenzao wanapata maslahi zaidi kuliko wengine.

Kuna madai kuwa UKAWA wamepatiwa fedha, tena nyingi na mfadhili ama wafadhili wa nje ya Tanzania, lakini fedha hizo zinaishia mifukoni mwa kiongozi mmoja ama wawili wa umoja huo, usiosajiliwa na unaoendesha shughuli zake za kisiasa, bila hati zozote za kuuhalalisha kuendesha shughuli za kisiasa.

Viongozi wa vyama CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vidogo vidogo walisusa Bunge Maalumu la Katiba mwezi uliopita, wakiazimia kuendesha kampeni ya kutafuta Katiba mpya nje ya Bunge, kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi. UKAWA walifanya mkutano wao wa kwanza mjini Zanzibar juzi.
Chanzo: Habarileo.

Thursday, May 1, 2014

KILIMO KWANZA


Friday, April 25, 2014

MAALIM SEIF; SIKUMMALIZA JUMBE.


NAIKUMBUKA KURA YA MAONI YA CCM YA MWAKA 1994 KUHUSU MUUNGANO

MJADALA wa Bunge Maalum la Katiba, hasa kuhusu muundo wa Muungano bado unavuta hisia za wengi kutokana na yanayozungumzwa.
Tunapoadhimisha miaka 50 ya Muungano huo, mambo mengi yanazidi kuelezwa, japo siyo mapya kwa vile yamekwishawahi kuelezwa katika Tume mbalimbali huko nyuma kama ya Jaji Robert Kisanga, Jaji Francis Nyalali na Jaji Joseph Warioba.

Mzee Warioba pia katika Tume ya Marekebisho ya Katiba aliwasilisha maoni kama yale yale, na safari hii yakiwa yametolewa mapendekezo lukuki ambayo kwayo ndiyo yaliyozaa mjadala mkubwa ndani ya Bunge Maalum.

Kubwa lililojitokeza ni kwa Wajumbe wengi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutamka hadharani kwamba wao wanataka muundo wa Muungano wa Serikali Mbili na siyo Tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Warioba.
Wengi wao wamekejeli hata takwimu zilizotumiwa na Tume hiyo kwamba siyo sahihi na hazibebi mawazo ya Watanzania wote ambao kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 wamefikia milioni 44.

Tuesday, April 22, 2014

BUTIJE: KIGOMA NI NYUMBANI WE HAVE TO RETURN TO


Tuesday, April 8, 2014

Siku 100 za mauaji ya Rwanda- 1994

ALLAH Ibariki Nchi Yetu 

Picha za watu waliouawa katika mauaji ya Rwanda mwaka 1994
Katika siku miamoja mnamo mwaka 1994, watu 800,000 waliuawa kinyama nchini Rwanda. Mauji hayo yalifanywa na wahutu wenye msimamo mkali.
Walikuwa wanawalenga watutsi waliokuwa wachache pamoja na wahutu wenye msimamo wa kadri.

Kwa nini wahutu waliwaua watutsi?

Asilimia 85 ya wananchi wa Rwanda ni wa kabila la Hutu, lakini jamii ya Tutsi imekuwa ikishikilia nyadhifa kubwa tu za ngazi za juu kwa miaka mingi.
Mwaka 1959, wahutu walimuondoa mamlakani mfalme wa Tutsi huku maelfu ya watu wa kabila hilo wakikimbilia nchi jirani kama vile Uganda.
Kikundi cha watutsi waliokuwa ukimbizini kikaunda vuguvugu waliloliita RPF ambalo lilivamia Rwanda mwaka 1990 huku vita vikiendelea hadi mwaka 1993 ambapo makubaliano ya amani yalifikiwa.
Lakini usiku wa terehe 6 Aprili mwaka1994, ndege iliyokuwa imewabeba hayati Rais Juvenal Habyarmana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira ilidunguliwa.
Kila mtu aliyekuwa katika ndege hiyo alifariki. RPF kilisema kuwa ndege hiyo iliangushwa na wahutu kama kisingizio cha mauaji kufanyika.

Waume waliwaua wake zao kwa hofu ya wao kuuawa

Mauaji ya Kimbari yalifanyika vipi?

Kwa mpangilio wa hali ya juu. Orodha ya majina ya waliokuwa wanapinga serikali ilitolewa kwa wapiganaji ili waweze kuwaua pamoja na familia zao.
Majirani waliuana na hata waume wa kabila ta Hutu kuwaua wake zao wa Tutsi wakisema kuwa wangeuawa ikiwa wangetaa kufanya hivyo.
Wapiganaji walitumia vitambulisho vya watu kuwaua kwani majina yao yalionyesha ikiwa walikuwa wahutu au watutsi. Maelfu ya wanawake walifugwa kama watumwa wa ngono


Jumuiya ya kimataifa ililaumiwa pakubwa kwa kutizama tu mauaji yalipokuwa yanaendelea Rwanda

Nani alijaribu kusitisha vita?

Umoja wa Mataifa na Ubelgiji zilikuwa na wanajeshi wao nchini Rwanda. Lakini umoja wa Mataifa haukuwa na idhini ya kusitisha mauaji.
Mwaka mmoja baada ya wanajeshi wa Marekani kuuawa Somalia, Marekani ilijitahidi kadri ya uwezo wake kujizuia kuingia katika vita barani Afrika.
Wanajeshi wa Ubelgiji walilazimika kuondoka nchini humo baada ya kumi kati yao kuuawa.
Walituhumiwa kwa kutofanya juhudi za kumaliza vita. Rais Paul Kagame ametuhumu Ufaransa kwa kuhusika na mauaji hao ingawa Ufaransa imekanusha vikali madai hayo.

Vita vilimalizika vipi?

Chama cha RPF kikisaidiwa na Uganda , kilianza kudhibiti sehemu kadhaa za nchi hiyo hadi Julai tarehe 4, wanajeshi wake walipoingia mjini Kigali.
Wahutu milioni mbili wengi wakiwa raia walikimbilia nchi jirani ya DRC wakihofia kushambuliwa kama hatua ya kulipiza kisasi.


Watu milioni mbili wa kabila la Hutu walikimbilia nchi jirani kuepuka kisasi cha watutsi

Vipi hali ya Rwanda sasa?

Rais Paul Kagame na chama chake RPF amesifiwa kwa kurejesha utulivu nchini Rwanda na hata kukuza uchumi wa nchi hiyo ndogo.
Pia amejaribu kuifanya Rwanda kuwa nchi inayong'aa kiteknolojia. Lakini wakosoaji wake wanasema kuwa hapendi kukosolewa huku vifo vya wapinzani wake vikileta shaka.
Takriban watu milioni mbili walihukumiwa katika mahakama za jadi, viongozi wa mauaji wakihukumiwa katika mahakama maalum kuhusu mauaji ya Rwanda mjini Arusha Tanzania.
Kwa sasa ni hatia kwa mtu yeyote kuzungumzia ukabila nchini Rwanda, serikali inasema hii inasaidia kuzuia kutokea tena kwa mauaji kama hayo, lakini wakosoaji wa serikali wanasema hiki ni kiini macho tu kwani hisia zilizopo kuhusu ukabila huenda zikasababisha hali nyingine mbaya baadaye ikiwa watu hawatapewa uhuru wa kuzungumza.

TAMKO LA CHADEMA KUPINGA UCHAGUZI MDOGO CHALINZE

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinatoa tamko la awali kwa umma kuhusu ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria zinazosimamia uchaguzi, zilizofanyika kwenye mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chalinze, ambao umehitimishwa Aprili 6, mwaka huu, kwa wapiga kura wa jimbo hili mkubwa kupiga kura.

Ukiukwaji huo ni kama ifuatavyo;

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza wapiga kura wapya kinyume cha sheria
Kinyume kabisa na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kifungu cha 15(5), kinachosema; 

“Kwa madhumuni ya kifungu hiki, Tume itapitia upya daftari la kudumu la taifa la wapiga kura mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na tarehe inayofuatia siku ya uteuzi,”
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekiuka kifungu hiki cha sheria kwa kufanya kile wanachoita wao ni ‘uhakiki wa mwaka 2014’ wa daftari ambao wanadai lengo lake lilikuwa ni kupunguza idadi ya wapiga kura waliokufa au kuhama au kuandikishwa mara mbili, lakini badala ya wapiga kura kupungua, uhakiki huo uliofanywa na tume bila kushirikisha wala kuwataarifu wananchi wa Jimbo la Chalinze, umeongeza idadi ya wapiga kura wapya katika jimbo hili kwenye uchaguzi huu mdogo.

Vile vile, kutokana na kitendo hicho cha NEC kuongeza idadi ya wapiga kura wapya kwenye daftari kimesababisha kuongezeka kwa vituo vya kupigia kura tofauti na ilivyokuwa mwaka 2010, ambapo Jimbo la Chalinze lilikuw ana jumla ya vituo 286 na sasa vimekuwa 288.

Kutangaza matokeo kinyume cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi >>>>

Sunday, March 30, 2014

WASIRA: BILA MUUNGANO HAKUNA CCM


Friday, March 28, 2014

TRENI YA MIZIGO YAPATA AJALI WILAYANI MPWAPWA MKOANI DODOMA

Treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar Es Salam kuelekea mkoani Kigoma imepata ajali saa 9 usiku wa kuamkia leo 28 March 2014 na kusababisha kifo cha mtu mmoja, wawili hawajulikani walipo na wengine sita kujeruhiwa

Ajali hiyo imetokea karibu na stesheni ya Gulwe iliyoko wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kusombwa kwa kipande cha njia ya reli na hatimae mabehea matano kuanguka.

Akithibitisha ajali hiyo katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Dr. Shaaban Mwinjaka amesema mafuriko hayo yalikuwa na mawimbi makubwa ya zaidi ya mita 4 kwenda juu yaliweza kukitupa umbali wa mita mia moja kichwa cha treni chenye uzito wa tani 80.

Dr. Mwinjaka amesema kwa sasa wanafanya taratibu za kukiondoa kichwa hicho na kurekebisha miundombinu iliyoharibika ili mabehewa ambayo hayakuanguka yaweze kuendelea na safari






BUNGE LA KATIBA LAPITISHA KURA MSETO KUFANYA MAAMUZI BUNGENI