Monday, January 7, 2013

WATOTO MKOANI KIGOMA WAPATIWA CHANJO YA PCV-13


ZAIDI ya Watoto 97,000  Mkoani Kigoma wamepatiwa chanjo  aina ya (PCV-13) dhidi  ya magonjwa Hatarishi  ya kuhara kukali,enomonia na uti wa mgongo ambao husababisha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kauli hiyo ilitolewa leo Kwenye kituo cha Afya cha Gungu Kigoma Ujiji ,ikiwa na tija ya kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kutoka  99% kwa  mujibu wa takwimu ya 2004  ya (Tanzania DemographicHealth Survey) ili  ifikapo 2015 iwe 90% ya vifo hivyo visiwepo, hali ambayo iliwashawishi wananchi kuitumia fursa hiyo kikamilifu ambapo watoto 97 ,000, walifanikisha zoezi hilo la chanjo dhidi ya magonjwa korofi ikiwemo kichomi, uti wa mgongo sanjari na kuhara kukali ambapo kunachochea kufariki kwa watoto  hao.
Akizindua chanjo hiyo Mkuu wa Mkoa Kigoma Lt.Issa Machibya alisema lengo la kuzindua utoaji wa chanjo hizo ni pamoja na kupiga hatua za kutokomeza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, kutokana na magonjwa ya kuhara na enomonia hali inayohatarisha kizazi cha leo na cha kesho katika mkoa wa Kigoma na kitaifa.
Machibya amesema anaipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuthibitisha kuwa chanjo aina ya`PNEUMOCOCCAL(PCV13)  kuwa ni salama hukinga nimonia kwa 38% na uti wa mgongo zaidi ya 87% ,alafu jamii hailipii  ni bure , pelekeni watoto waepukane na adha ya magonjwa hatarishi msisikilize wazushi eti msiwapeke hawawatakii mema vijana wetu.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Leonard Subi amesema kuwa,2009 chanjo zilikuwa zikitolewa dhidi ya magonjwa nane lakini  leo chanjo hutolewa dhidi ya magonjwa 11  baada ya kuongezeka chanjo mpya 2(PCV-13) ambazo zinakidhi kudhibiti maradhi hatarishi ya kuhala kukali,kichomi na uti wa mgongo
CHANZO: Magreth Magosso,Kigoma

No comments:

Post a Comment