Monday, March 18, 2013

MSAFARA WA RAIS WAUA ASKARI WA USALAMA BARABARANI DAR.


"Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.

Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:

Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.

Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.

Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu"

CHANZO: JAMII FORUM

1 comment:

  1. Taarifa ya Polisi: Mtu aliyeendesha gari Landrover Discover T328 BML rangi nyeusi mali ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) na kuufukuzia msafara wa Rais na kusababisha kifo cha askari polisi WP Elikiza Nnko amekamatwa na Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam

    ReplyDelete