Thursday, January 24, 2013

VYUO VYA UDSM, MKWAWA NA CUJ- DAR VYAONGOZA KWA UKAHABA

UDSM
MKWAWA




WANAFUNZI wa vyuo vikuu, hasa vya Dar es Salaam, Mkwawa Iringa na Chuo cha Ustawi wa Jamii cha Dar es Salaam, vimeonekana kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofanya biashara ya ngono kuliko vyuo vingine nchini.
Hayo yalibainishwa na Mratibu Msaidizi wa Kudhibiti Ukimwi wa Manispaa ya Iringa, Gaspar Nsanye, alipozungumza na wadau mbalimbali katika mdahalo wa siku mbili kuhusu mpango mkakati wa AMICAAL kuhusu makundi yaliyosahaulika katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na ukimwi na kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo, madiwani, wakurugenzi na wadau waliopo mkoani hapa.
Alisema matokeo ya zoezi la kupata maoni na hali halisi ya makundi maalumu yalionesha kuwa baadhi ya makundi yapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya mashoga, wanaotumia dawa za kulevya, watoto wa mitaani, wafungwa pamoja na wanaofanya biashara ya ngono.
“Hivi sasa kuna kasi kubwa ya kukua kwa makundi hayo na yanaelekea maeneo mengine hasa mijini na idadi ya watu wanaopata maambukizi mapya katika makundi haya inaongezeka,” alisema Nsanye.
Alisema sababu hasa zilizotajwa za watu kujiingiza katika makundi hatarishi ni pamoja na utamaduni katika baadhi ya maeneo kama Tanga na Zanzibar, umaskini na matatizo hasa kwa wafungwa, uchangiaji wa vifaa kwa wanaojidunga dawa za kulevya na ngono isiyo salama.
Alisema miongoni mwa mikakati iliyowekwa na Manispaa ya Iringa ni kuongezwa kwa vituo vya huduma ya afya kwa walioathirika na dawa za kulevya na ukimwi na kutoa elimu jinsi ya kufanya ngono salama, kuendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya kondomu kwa watumishi, wanafunzi, vijana na kusambaza kondomu kwenye baa, kata vyuoni na katika jamii.

CHANZO: T/Daima.

No comments:

Post a Comment