Tuesday, March 5, 2013

MORINHO: DUNIA ITASIMAMA 90' KUSHUHUDIA MECHI KATI YA REAL MADRID NA MAN U.

Kocha mkuuwa Real Madrid Jose Morinho amesema mechi ya leo kati Real Madrid na Manchester United itakuwa ni ngumu  kwa kuwa timu zote mbili zina washambuliaji wazuri.

Morinho amesema Man U imeshinda  mechi zake mbili zilizopita katika kombe la ligi na kombe la na kombe la FA hatua ya robo fainali na wao wamepoteza mechi moja kati ya mechi 12 zilizopita hivyo dunia itasimama kwa dakika 90 kushuhudia mtanange kati ya timu hizo mbili.

"Ni jambo zuri wakati kuja kwenye mechi na wachezaji wakiwa katika hali ya kujiamini" amesema Morinho wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Old Trafford ambapo mechi hiyo itachezwa kuanzia majira ya saa 4:45 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Wiki mbili zilizopita timu hizo zilishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya goli moja kwa moja katika mchezo ambao Madrid alikuwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment