Friday, March 8, 2013

MAMA SALMA KIKWETE ATOA UJUMBE KWA WANAWAKE KUPITIA FACEBOOK


MKE wa Rais Mama salma Kikwete ametoa salam zake kwa wanawake wote duniani na kuwatakiwa maisha mema na yenye baraka katika.Mama Salam alitoa salam hizo kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alisema "Leo ni siku ya wanawake Duniani,ni siku ya kujitazama kama Taifa juu ya hali ya wazazi hawa na walezi wa Taifa hili".

"Ni siku ya kujipima na kutathimini namna gani, wanawake wamewezeshwa kujitambua na kushirikishwa katika mipango ya maendeleo ya jamii yetu. Tunapofikiri kama Taifa ni namna gani tunaweza kujikomboa katika Umasikini tulionao ni lazima mipango hiyo iende sambamba na mipango na mikakati ya ukombozi kwa wanawake wa Taifa hili"aliongeza Mama Salma.

Maadhimisho hayo yamefanyika duniani kote ambapo Tanzania yalifanyika kila mkoa, huku jijini Mwanza yakifanyika katika viwanja vya Nyamagana.

No comments:

Post a Comment