Mwili wa mwanamke mwanafunzi wa chuo cha St John Dodoma ukiondolewa eneo la tukio mjini DodomaTANGANYIKA ONEimepokea taarifa
kutoka Dododma zikieleza kuwa Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu
cha St John Dodoma aliyekuwa anasoma fani ya Unesi amekutwa akiwa
amekufa katika eneo la chuo hicho leo asubuhi.Taarifa za awali zimeeleza kuwa baada ya polisi kufika katika eneo hilo walishuhudia mwili huo ukiwa kama ulivyozaliwa(hauna nguo) na nguo za mama huyo anayedaiwa kuwa na zaidi ya miaka 40 zikiwa pembeni mwa mwili wake.
Taarifa zimeendelea kusema kuwa baada ya kukagua mwili huo imebainika kuwa mama huyo alibakwa na watu wasiojulikana hadi kufa na kutokana na suala hilo inadaiwa kuwa mkuu wake mmoja umekatwa.
Kitendo cha mguu wa marehemu huyo kukatwa imezua utata zaidi kwani haikujulikana mara moja kama ulikatwa na wanyama wa mwituni watuhumiwa wa mauaji hao
Polisi imeeleza kuwa inafanya uchunguzi mkali ilikuweza kuwabaini watu waliohusika katika sakata hilo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment