Thursday, March 14, 2013

POLIS KIGOMA WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUSAMBARATISHA MAANDAMANO YA MADEREVA WA BODABODA

Na Magreth Magosso,Kigoma.
 
Polis Mkoani Kigoma wamelazimika kutumia Mabomu ya machozi ili kuwatawanya waendesha  Bodaboda wa  Manispaa ya  Kigoma Ujiji, baada ya kufanya maandamano  ya kutaka askari wa barabarani wasitumie nyadhifa zao kwa maslai yao binafsi.
 
Kauli hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa waendesha Bodaboda Fikirini Shaban eneo la maweni, kudai kuwa,askari hao wana tabia ya kuwasimamisha waendesha bodaboda si kwa tija ya kuwakosoa na kuwaelimisha kwa makosa husika, bali hutaka kiasi cha fedha kuanzia 10,000 hadi sh.5,000  ili uendelee kufanya kazi,la ukikataa kusimama watakuandama kwa kufukuzana nao barabarani hali inayosababisha ajali zisizo tarajiwa.
“Baadhi ya abiria hukataa kuvaa kofia ,lakini askari akikusimamisha na ukisimama wanatoza fedha isiyo na tija kwa serikali huweka mifukoni mwao jana ajali ilitokea  na kujeruhi watu watatu kisa hakusimama baada ya askari kumsimamisha kwa kuhofu kutolewa  sh.10,000 ukibana sana unatoa 5,000 eti ya mafuta tena hakuna risiti” alibainisha  Kaopa Denis mwendesha pikipik.
Mganga Mkuu wa Kigoma Leonard Subi alikiri Hospitali yake  jana ilipokea majeruhi wa ajali hiyo na kubainisha kuwa, waliolazwa hadi sasa wapo watatu ambao hali zao si za kuridhisha.
 
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Dismas Gapikisusi alidai kuwa,tukio hilo bado linafanyiwa mkakati wa kuweza kulitolea jibu maalum na kumtaka mwandishi wa gazeti hili asubiri siku wandishi wa habari watakapoitwa ili abainishe ukweli wa mambo.
Wakati huohuo baada ya waendesha bodaboda kufanya mandamano hayo sanjari na kutupa   jaketi za kuakisi mwanga kituo cha polisi kati Kigoma, Waendesha pikipiki wanne wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Kigoma kwa kosa la kufanya fujo polisi leo.

No comments:

Post a Comment