Wednesday, January 30, 2013

LULU HUYOO!! ATINGA URAIANI



Lulu na mama yake wakimwaga machozi baada ya kukutana nje ya Mahakama Kuu
 Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael (Lulu) ameonana na Msajili wa Mahakama Kuu Amir Msumi na kusaini hati ya dhama kisha kuondoka na mama yake mzazi kurejea nyumbani.
Msanii huyo alishindwa kuzuia furaha yake na kumwaga machozi baada ya kukumbatiana na mama yake mzazi huku baadhi ya watu waliofika Mahakamani hapo pia wakifurahia kuachiliwa kwake kwa kumwaga machozi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mahakamani hapo Lulu alisema kwamba anamshukuru Mungu kmpatia nafasi ya kurudi nyumbani na kuungana na familia yake.
"Kwakeli sina chakusema kwa leo zaidi ya kumshukuru Mungu kwani bila yeye nisingepata hii dhamana ya kurudi nyumbani na kuonana na mama yangu"alisema Lulu.
Akisoma uamuzi wa maombi ya dhama ya msanii huyo Jaji Mruke alisema, "Mahakama imekubali maombi yako ya dhamana na uko huru kwa masharti yafuatayo, (moja) unatakiwa kuwasilisha gharama zote za safari ndani ya jiji la Dar es Salaam".


"(Pili) usisafiri nje ya Dar es Salaam bila idhini ya Msajili wa Mahakama Kuu, (tatu) unatakiwa kuripoti (kujiwakilisha) kwa Msajili wa Mahakama kila tarehe mosi ya kila mwenzi".
Akisoma uamuzi wa maombi hayo Jaji Mruke alifafanua kuwa, "Sharti la (nne) unatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini na wawe na tsh 20milioni kila mmoja".
"(Tano) ni kwamba unatakiwa kutimiza masharti ya dhamana na kusaini mbele ya msajili wa Mahakama na utaendelea kubaki rumande mpaka utakapotimiza masharti yote"


1 comment:

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    ReplyDelete