Sunday, January 27, 2013

ZITO: SERIKALI IMECHANGIA MAUAJI MTWARA


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe  ameishutumu serikali kuwa ndio chanzo cha mauaji ya Mtwara kwani imeshindwa kusimamia amni mkoani humo
Akizungumza na waandishi wa habari zito amesema mauaji hayo yametokea kwa sababu serikali imeshidwa kusimamia na kutekeleza utawala bora.
"Hali inayoendelea huko Mtwara ni hali ya kusikitisha,vurugu,mauaji na kuharibu mali kamwe siyo utanzania"amesema Zitto.
Zitto amefafanuwa kuwa, Hatuwezi kuendelea kurushiana lawama ilhali nchi yetu inaungua,serikali na wanasiasa wote tuhakikishe kuwa tunatimiza wajibu wetu kwa kusikiliza wananchi na kufanyia kazi matakwa yao.
Kufuatia vurugu za jana watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa huku mali mali za serikali na za baadhi ya viongozi zikiharibiwa na wananchi. miongoni mwa waliojeruhiwa ni dereva mmoja wa bodaboda aliyepigwa na polisi hadi kuzirai kwa tuhuma za kuhusika katika uchomaji wa jengo la mahakama ya mwanzo na mwandishi wa habari wa Chanel Ten aliyepigwa jiwe kisogoni.
Mbali na uteketezaji wa malimza serikali nyumba ya Mh. Hawa Gasia ikivunjwa vioo na kuchomwa motto wakati ile ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa vioo
.vurugu hizo zinahusisha na sakata la GESI kwani Hawa Gasia na Sinani wamekuwa kwa Muda Mrefu wakishutumiwa kwa kuchochea na kuridhia usafirishaji wa gesi hiyo kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam
 

No comments:

Post a Comment