Na Magreth Magosso : Kigoma
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila amewataka wananchi wa jimbo lake,watarajie ujio wa mitambo na mashine ya kuchimba visima ifikapo April Mwaka huu ili kupunguza adha ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa miongo 13.
Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma ya Wanawake wa kijiji
cha Kabuyange kata ya Ilagala Jimbo la Kigoma kusini kumshutumu Mbunge
huyo kwa kuwatelekeza na adha ya maji ambayo inawakabili kununua maji
hayo, ambapo dumu la lita 20 huuzwa kwa sh.150 zaidi ya miaka 13.
Kafulila aamekiri jimbo lake linakumbwa na kadhia hiyo,ingawa alidai adha
ya maji ni katika wilaya sita za mkoa wa kigoma ,ambapo zinazopata
huduma hiyo ni 27% tu,huku akibainisha mkakati wa kufanikisha kupunguza
adha hiyo April 2013,pindi mitambo na mashine zitakapowasili kutoka kwa
wadau wake Nchini China .
"kweli wananchi wanateseka hasa kinamama ambao huathirika na zoezi
la utafutaji wa maji kwa umbali mrefu huku baadhi ya watoto wa kike
wakipata mimba kwa kusubiri foleni ya maji, ya kisima kimoja tu kijijini
hapo,nawananchi waliowengi hushindwa kumudu ununuzi wa maji,kutokana na
hali ngumu ya kimaisha" alisema Kafulila.
Aidha alidai kuwa,ili kumaliza tatizo la maji katika mkoa wa kigoma
ni pamoja na kutumia mto malagarasi kwa kutandaza mtandao wa maji,ambao
utasaidia kwa asilimia miamoja kigoma kuondokana na kadhia hiyo.
Akizungumzia kadhia hiyo Madina Abeid (mwananchi) amesema,wamekuwa wakiitwa kwenye vikao vya kijiji ili kuelezea
changamoto zinazowakabili katika kijiji hicho,ikiwemo kero ya maji na
walishachangishwa sh.3,000 lakini haipatiwi ufumbuzi wa aina yeyote na
wakijaribu kumhoji mtendaji wa kijiji fedha zilipo adai amepeleka ila
hajui hatma yake..
"mimi sielewi kabisa hii shida ya maji itaisha lini hapa
kabuyange,kisima kipo kimoja kiangazi hii maji ya foleni ,hivyo
tunanunua maji ya m to malagalasi serikali nayo kupitia halmashauri wako
kimya shida yetu" alisema kwa huzuni Abeid.
Hamisa Nungu aliongeza kwa kubainisha kuwa,wananchi walifarijika
kumpata kiongozi kijana ambaye atasaidia wazazi wake waondokane na
kadhia hiyo ya miaka kenda,lakini huzuni ya kusaka maji kila kukicha
katika kijiji cha ilagala imebaki kuwa sugu.
Kutokana na mkakati wa Mbunge huyo,wananchi wa kata hiyo wasubiri
mkao wa kunufaika na ujio wa mitambo na mashine za uchimbaji wa visima
kulingana na maeneo yenye uwepo wa maji ikiwa ni sehemu ya kupunguza
kadhia hiyo.
No comments:
Post a Comment