Thursday, January 24, 2013

WANANCHI WA KIBITI WACHOMA NYUMBA ZA ASKARI POLISI


Wananchi wa Kibiti wilayani Rufiji wakichoma nyumba za askari polisiWanachi wenye hasira kali leo wamevamia kituo cha Polisi cha Kibiti Wilaya ya Rufiji na kufanya vurugu zenye kubwa kiasi cha kutaka kukichoma moto baada ya kugundua kuwa mwenzao amekufa baada ya kupigwa na polisi.

Katiak vurugu hizo wananchi walikuwa na mapanga, marungu na wengine kushika matairi ya magari wakitaka kuchoma kituo hicho.

Inadaiwa kuwa polisi wa kituo hicho walimpiga Hamisi Mponda nakumsababishia majeraha na kuvuja damu nyingi kitendo ambacho kilimfanya alazwe katika hospitali ya Muhimbili na kufariki baadae.

Askari wengi walitanda  katika kituo hicho, wananchi hao wamebadili hicho na kuwafanya wanachi wabadili utaratibu na kuamua kuzichoma nyumba za askari hao zilizopo pembezoni mwa kituo hicho bila kuhofu kitu chochote kinachoweza kuwadhuru.

No comments:

Post a Comment