Friday, January 25, 2013

WASIRA: UCHIJAJI WA NYAMA YA BIASHARA UTAFUATA MFUMO AMBAO HAUTALETA MTAFARUKU KATIKA MADHEHEBU YOTE YA DINI

Hatiame mkutano wa usuluhishi na wa amani kati ya makundi mbalimbali aya kidini juu ya ikhtilafu za uchinjaji umemalizika kwa waumini wa madhehebu ya kikristo kuruhusiwa kuchinja katika hafla za kibinafsi na yule anataka kuchinja kwa ajili ya biashara achinje katika mfumo ambao hautaleta tafrani baina ya waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali.

Katiaka tamko la maafikiano lililotolewa na waziri wa nchi ofisi ya rais mahusiano na uratibu Mh. Stevine Wasira amesema machinjio ya serikali yataendelea kusimamiwa katika utaratibu uliokuwepo toka awali na wakristo wanaruhusiwa kuchinja vichinjwa binafsi na si vya biashara.

Waziri Wasira amesema maafikiano hayo yamefikiwa kwa lengo la kudumisha amani, utulivu na mshikamano wa watanzania.

Wakiongea na waandishi wa habari baada kikao hicho baadhi wa viongozi wa madhehebu ya kikristo hawakukubaliana na maafikiano hayo na kudai kuwa uamuzi uliofikiwa ulikuwa wa kisiasa zaidi na kukishutumu Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali kuwapendelea waislam.

Viongozi wa Madhehebu ya kikristo wamedai kuwa suala la kuchinja ni ibada kwa waislam na wanapolazimishwa kula nyama inayochinjwa na waislam ni sawa na kuwalazimisha wakristo kufanya ibada ya kiislam mkitu ambacho hawako tayari kukikubali.

Kwa upande wa viongozi wa madhehebu ya kiislam wamekubaliana na maafikiano walioafikiana katika kikao hicho.

Waziri wasira amewataka viongozi wa dini zote kuisaidia serikali katika kuwahimiza watanzania kufuata sheria bila kushurutishwa.

No comments:

Post a Comment