Wednesday, January 23, 2013

WANAFUNZI WA AMITIER SEC. WANATUHUMIWA KWA MAUAJI


 
,Na Magreth Magosso,Kigoma,
 
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya `AMITIER’ iliyopo katika kambi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma,wanasadikiwa kufanya mauwaji ya Tona Kabwe(63) kwa kumtuhumu kuwa ni mchawi. na walimu wao wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani hapo.
 
Taarifa hiyo imetolewa na ACP Frasser Kashai alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwakwe Kigoma Ujiji jana, alisema 22,Januari,2013 saa 4.20 kwenye kambi ya wakimbizi ya nyarugusu wanafunzi hao wakiwa pamoja na walimu wao,walikwenda nyumbani kwa marehemu kwa tija ya kutoa pole baada ya kufiwa na mjukuu wake ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.
 
"inasemekana wanafunzi hao awali mjukuu wa marehemu ambaye naye alifariki baada ya kuugua kwa siku chache hivi karibuni ,inasadikiwa kabla ya kifo chache aliwahadithia baadhi ya wanafunzi wenzie juu ya ndoto yake aliyomuota babu yake akimrisha nyama hali iliyowajengea imani wanafunzi hao kwenda kulipiza kisasi kwa babu huyo kwa kumpiga na fimbo sanjari na kuni hadi umauti ulipomfika" alisema Kashai.
 
Alidai kutokana na tukio hilo Jeshi la polisi linawashikilia walimu wane wa shule hiyo kwa upelelezi ,huku akitoa rai kwa wananchi wapunguze imani za kishirikina.Wakatihuohuo 22,Januari,2013,saa 10 jioni kijiji cha kwaga wilayani kasulu watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni mke na mume Hakani (45) na Prisca William wamekufa baada ya kupigwa na radi wakiwa shambani.
 
Muguzi wa zahanati ya Kwaga Leonard Haiki alipohojiwa na wandishi uwepo wa taarifa hiyo,alikana kufa kwa Prisca huku akidai kufa riki kwa mumewe Hakai, na kubainisha majeruhi watano ambapo watatu wamepelekwa kituo cha afya cha Kasulu. Wakati huohuo kijiji cha Nyarugusu saa 4.00 mtoto Sharifu Rajabu (15) amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba ya chandarua chumbani kwakwe .
 
Kashai alidai chanzo cha kujinyonga kwake ni kitendawili na upelelezi bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment