Thursday, January 24, 2013

WAZIRI MKUU ATAKA MADARAKA YA RAIS YAPUNGUZWE


Waziri mkuu wa jamuhui ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ametaka Katiba Mpya impunguzie Rais madaraka hasa katika nafasi ya uteuzi.
Pinda ametoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba iliyoko katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya watanzania juu ya katiba mpya.

Kauli hiyo ya Pinda inapingana na ile iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuhusu Katiba Mpya ambaye aliiambia Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba madaraka ya Rais yasiguswe akisema kama atanyang’anywa, atashindwa kuongoza nchi.
Balozi Sefue alisema nafasi ya Rais inapaswa kuwa imara na yenye uwezo wa kuwaunganisha Watanzania wote.

Pinda amebainisha kuwa kuna haja ya kumpunguzia Rais madaraka kwani amekuwa na mzigo mkubwa wa kuongoza Serikali, "kitu kikubwa ambacho ningependa kiangaliwe kwenye Katiba Mpya kwa upande wa madaraka ya Rais ni katika uteuzi wa viongozi mbalimbali.”

"Nimetaka Katiba Mpya impunguzie mzigo Rais kwani amekuwa na kazi nyingi sasa ni vyema angepunguziwa mzigo huo hasa katika masuala ya uteuzi wa viongozi.”
Pinda alitoa mfano kwamba katika kazi ya uteuzi wa viongozi, Makamu wa Rais anaweza kumsaidia kazi hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine ambavyo Katiba itaviainisha.

No comments:

Post a Comment