Thursday, October 10, 2013

KANISA KATOLIKI NCHINI UJERUMANI LATAKA WALIOOA AU KUOLEWA NDOA YA PILI WARUHUSIWE KUPOKEA SAKRAMENT

 Jimbo Kuu la kanisa katoliki la Freiburg nchini Ujeruman limetaka limetaka wanaume au wanawake walioa au kuolewa katika ndoa ya pili waruhusiwe kupokea sakrament ya ekaristi takatifu na zingine.

Jimbo hilo wiki hii limetoa kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mapadri wanaofundisha Wakatoliki waliooa mara ya pili (mitala) kuelezea masitikiko kama njia ya toba kwa kushindwa kuendelea na ndoa ya kwanza ili waruhusiwe kupokea sakramenti ya ekaristi takatifu na nyingine.


Maaskofu nchini Ujerumani wamekuwa wakitoa maombi mara kwa mara kuiomba Vatican iruhusu watu kutengana na kuruhusiwa kuoa au kuolewa mara ya pili katika miaka ya hivi karibuni kufuatia waumini waliooa mara ya pili au kutoolewa mara ya pili kuhudhuria misa, lakini wakiwa hawaruhusiwi kupokea sakramenti ya ekaristi.

Kitabu hicho cha mwongozo kimesisitiza kuwa Wakatoliki wanapaswa kukubali kuwa kuna ndoa ambazo hazijafanikiwa, zimeshindikana, hivyo wanapaswa kuzijadili na mapadri wao, lakini waoneshe kwa imani kuwa watakuwa waaminifu kwa ndoa zao za pili na ni haki yao kuwa na familia za aina hiyo.

 .
Kwa upande mwingine Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani (Vatican), yamewaonya maaskofu kutofanya mageuzi ya haraka kabla ya kupata baraka za kiongozi wao, Baba Mtakatifu Francis.

Onyo hilo lilitolewa juzi baada ya Dayosisi ya Ujerumani kusema kuwa wanandoa walioachana na kuoa tena, kanisa hilo sasa litawaruhusu kupokea sakramenti ya ekaristi na sakramenti nyingine.
Msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi, alisema kuwa Papa Francis atafanya sinodi maalumu ya maaskofu Oktoba mwaka 2014 kujadili masuala yanayoikabili familia.

Alisema kuwa hatua ya makanisa kujitangazia mageuzi yao wenyewe inaweza kusababisha mkanganyiko siku za usoni.
Inavyoonekana Papa Francis anaweza kutilia maanani changamoto zinazojitokeza kwa mujibu wa sheria za kanisa, hasa kuhusu watu waliooa kwa mara ya pili kuruhusiwa kupokea sakramenti ya ekaristi.
Papa Francis alionekana kukubali uwezekano wa mabadiliko katika sheria za kanisa zinazowakataza watu waliooa au kuolewa kwa mara ya pili kutoruhusiwa kupokea sakramenti kwa kuzingatia kuwa vifungo vya ndoa havitenguliwi, jambo ambalo maaskofu wengi wanaliona kuwa tatizo kubwa katika majimbo yao.


Msemaji wa Papa, Kardinali Lombard, alisema Papa Francis hakuzungumzia mwongozo wa kitabu hicho cha Jimbo Kuu la Freiburg, lakini alisisitiza kuwa alifanya majadiliano na maaskofu wake kuhusu namna ya kufanya mabadiliko katika kanisa.
Papa Francis ambaye ni mzaliwa wa Argentina, amelitikisa kanisa tangu kuchaguliwa kwake Machi mwaka huu kwa kuelekeza mabadiliko zaidi kwenye masuala ya msamaha kuliko ya utoaji mimba na ndoa za jinsia moja, mahali ambako ndiko kuna changamoto za wazi kwenye mafundisho ya kanisa hilo.
Hata hivyo, Papa anaonekana kupokea ushauri wa wasaidizi wake kwa karibu na wamesisitiza mara kadhaa kuwa mabadiliko hata kama yatatokea yatachukua muda kufikiwa.

Askofu Mkuu wa Freiburg, Robert Zollitsch, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Ujerumani, alipokea mitazamo miwili tofauti wiki hii.
Mitazamo hiyo kwa mujibu wa Alis Glueck, Rais wa Kamati Kuu ya Wakatoliki nchini humo, ilijihusisha hasa na hoja ya kuonesha ni namna gani watu walio makini katika maisha yao ya imani wanaweza pia kutumia muda wao kushiriki katika maisha ya kanisa.

Kardinali wa Munich, Reinhard Marx, mmoja wa makardinali wanane walioteuliwa kama washauri wa Papa, alikiita kitabu hicho cha mwongozo cha Freiburg kuwa ni “mchango katika mjadala usiokwisha” na kusisitiza kuwa suala hilo litatatuliwa kwa manufaa ya kanisa zima ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment