Saturday, October 12, 2013

TANGANYIKA ONE: STOP, UDHALILISHAJI DHIDI YA WANAWAKE

Tanganyika One imesikitishwa na kitendo kitendo kilichotokea nchini Kenya cha wanaume watatu waliombaka msichana mmoja na kutupa mwili wake kwenye choo huku jeshi la polisi nchini humo likiwaamrishwa wanaume hao kukata nyasi kama adhabu ya kosa walilofanya.

Udhalilishaji na unynyasaji huu wa wanawake umekuwa ukitokea maeneo balimbali duniani hususan barani Afrika haukubaliki na ni kinyume cha sheria za haki za binadam na kinaondoa utu na hadhi ya mama zetu, dada zetu, wake zetu, nk

Kwa kutambua hadhi ya mwanamke na mchango wake katika maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni TANGANYIKA ONE inaomba watu wote kuungana katika kukomesha vitendo vyote vya udhalilishaji kwa wanawake.

Ikumbukwe kuwa Msichana huyo alishambuliwa na kubakwa akiwa njiani kutoka kwenye mazishi ya babu yake katika kijiji kimoja Magharibi mwa Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Daily Nation nchini Kenya, uti wa mgongo wa msichana huyo ulivunjika wakati wa ubakaji na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu pamoja na wabunge wamelaani polisi kwa kukosa kuchunguza madai ya msichana huyo.

Msichana huyo alinukuliwa akisema kuwa anataka waliomfanyia kitendo hicho kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Idara ya polisi inawachunguza polisi waliopokea malalamishi ya msichana huyo , alisema Halima Mohammed , kamanda wa polisi katika jimbo la Busia ambako kitendo hicho kilitokea.

TANGANYIKA ONE  inavitaka pia vyombo vya dola kuwachukulia hatu za kisheria wale wote wanaoshiriki kuvua utu wa mwanamke.

No comments:

Post a Comment