Saturday, October 12, 2013

WILSHERER: WAINGEREZA PEE NDIO WAICHEZEE ENGLAND

Mchezaji wa kiungo wa Arsenal na England amezusha mjadala kuhusu matamshi yake kwamba Waingereza tu ndio waiwakilishe timu ya soka ya England.

Jack Wilshere alikua akielezea msimamo wake baada ya kijana wa Manchester United Adnan Januzaj kutajwa kwamba anaweza kuichezea England ikiwa atatimiza masharti ya Fifa ya ukaazi wa miaka 5 kwa kua bado hajaamua alichezee taifa gani.
Januzaj, mwenye umri wa miaka 18, ana haki ya kuchezea Ubelgiji, Serbia, Albania na Uturuki.
Alipoulizwa kuhusu hilo , Wilshere alijibu: "Kuishi England kwa miaka mitano haikufanyi kua Muingereza."
Baadae akiandika katika mtandao wa jamii wa Twitter alisema matamshi yake hayakumkusudia Januzaj.

"swali lilikua wachezaji wageni waruhusiwe kuichezea England, na kwa maoni yangu sidhani waruhusiwe. Yeye ni mchezaji hodari lakini si Muingereza."

No comments:

Post a Comment