Saturday, October 12, 2013

AU WAKUBALIANA UHURU ASIHUDHURIE ICC



Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya asihudhurie kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, ila ikiwa itaakhirishwa.
Katika azimio lao viongozi wa Afrika walisema kuwa kiongozi yeyote wa taifa asitakiwe kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko madarakani.
Kesi ya Rais Kenyatta ambaye anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu inatarajiwa kuanza mwezi ujao mjini Hague, ingawa ameomba mara kadha kwamba iakhirishwe.
Bwana Kenyatta siku zote amesema kwamba atashirikiana kikamilifu na ICC.
AU inaishutumu ICC kuwa na kigeugeu - kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.
Hapo awali Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, alisema kesi za ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Omar al-Bashir wa Sudan zinaweza kuzuwia juhudi za kuleta amani na mapatano katika nchi zao.
Mkutano umemalizika.

No comments:

Post a Comment