Timu ya CHADEMA kanda ya Magharibi ikijumuisha Mwenyekiti wa Kanda Ndg.
Mambo na Wenyeviti wa Mikoa 3 ya Kigoma, Tabora na Katavi tumetembelea
Jimbo la Bukene, wilaya ya Nzega.
Kama ilivyo kwa mikutano iliyopita tumezungumza umuhimu wa Katiba na
mchakato wake kutopendelea chama chochote cha siasa kwani tunaandika
katiba ya nchi, umuhimu wa mwafaka wa kitaifa na kuwapongeza viongozi
tuliwaambia wananchi wasikubali mbinu chafu za kutaka kuongeza muda wa
Bunge mpaka 2017 kwani itakuwa ni kinyume na katiba yenyewe.
Wananchi wa Bukene ni wakulima wa Pamba na sehemu kidogo Tumbaku. Kioja
tulichokikuta Bukene ni wananchi kuuziwa dawa za Pamba feki ambazo
haziui wadudu! Wananchi wa vijijini wanafanyiwa kila aina ya dhulma na
kukandamizwa.
Pia tulielezwa namna watendaji wa vijiji na kata wanavyonyanyasa raia
kwa kujifanya wao wakamataji, waendesha mashtaka na mahakimu. Wanatoza
faini wananchi kwa kesi za kubambika. Itabidi tutafute namna ya
kuhakikisha hatua zinachukuliwa dhidi ya watendaji wa kata na vijiji
wanaokiuka misingi ya utawala bora. Wananchi wa vijijini wana haki ya
kuishi kama raia wengine wa Tanzania. Tusiwasahau
No comments:
Post a Comment