Serikali
imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi
nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani
bajeti iliyopo haitoshi.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo,wakati akizungumza na
wanafunzi waliokosa mikopo ambapo kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi
wizarani hapo.
"Kasungura kadogo na mkumbuke kuwa mkopo
ni kuomba kuna kupata na kukosa...hivyo wale waliokosa na walikuwa na vigezo
watafute watu wengine wenye uwezo wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata
watume tena maombi," alisema.
Alisema kilio chao
amekisikia na leo atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na
malalamiko yao ambapo suala hilo litapelekwa Bungeni ili kujadiliwa.
"Kama Bunge litaamua kupunguza fedha
kutoka kwenye bajeti zingine ili kusomesha wanafunzi hao. Bunge litaamua kwani Serikali
ina nia nzuri sana
kwani hadi sasa imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu hawarudishi,"
alisema.
Alitaja sababu
nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia uhitaji, kwani kuna
masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu wa wataalamu.
Alitaja fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na
wahandisi. Alitaja sababu nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni waombaji
kukosea majina na vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa kwenye vyombo
vya habari warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.
Alisema waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa
6,000 lakini waliorudi kufanya marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000
walikuwa na vigezo lakini wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).
Wanafunzi waliokosa mikopo walisema kama
wenzao wameweza kupata mikopo kwa asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana
ili wote waweze kupata
No comments:
Post a Comment