Wednesday, October 9, 2013

WAKATI PINDA AKIPOKEA MSHAHARA WA MILIONI 26 KWA MWEZI, BAADHI YA WALIMU NA WANAFUNZI WANAJISAIDIA VICHAKANI KWA KUKOSA VYOO

 
Wakati Waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (mtoto wa mkulima) akipokea Tsh 26 Milioni kama mshahara wake wa mwezi wanafunzi wa shule ya msingi Majengo mkoani tabora wanajisaidia vichakani kwa kukosa nyoo tangu kuanzishwa kwake 2007.
"Pinda anapokea sh mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya waziri na kiasi kinachosalia kufikia sh mil. 26 kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu" alisema Zitto Kabwe ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Zitto alitaja mshahara huo juzi mjini Mpanda na jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama

Wakati hayo yakijiri Shule ya Msingi Majengo, iliyopo katika Kata ya Usinge, wilayani Kaliua,Tabora, haina vyoo vya wanafunzi wala walimu tangu ianzishe mwaka 2007.
 Hayo yameelezwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo, Regena Luhende,  kupitia katika risala yake kwa Mbunge wa Kaliua, Prof Juma Kapuya aliyekwenda  shuleni hapo kukagua shughuli za maendeleo
Mwalimu Luhende alisema  shule inakabiliwa na  tatizo la kukosa vyoo tangu kuanzishwa kwake na kwamba hali hiyo inawafanya walimu na wanafunzi wao, kujisaidia vichakani.
Aliiomba Serikali na wadau wengine wa elimu mkoani Tabora, kutoa msaada wa fedha ili kugharimia ujenzi vyoo katika shule hiyo.
Pia alisema shule yake inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati, jambo linalosababisha wanafunzi kuketi sakafuni wakati wa kusoma.
 Kwa upande wake, Profesa Kapuya alitoa mchango wa Sh3milioni   kwa shule hiyo na kuuagiza uongozi  kutumia fedha hizo, kujenga vyoo.

No comments:

Post a Comment