Wanajeshi wa DRC wakishirikiana na vikosi vya MONUC vinavyoongozwa na wanajeshi wa Tanzania wamefanikiwa kuwaondoa waasi wa
M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana mpakani na Uganda
Mji wa Bunagana umekombolewa
kufuatia makabiliano makali adhuhuri ya jana ambapo baadhi ya waasi
walilazimika kuimbilia msituni huku baadhi yao wakidai waliingia Uganda wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia
Msemaji wa serikali alisema kuwa mji wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa serikali.
.
Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23 wanaopambana dhidi ya serikali ya DRC huku wakidaiwa kusaidiwa na serikali ya Rwanda.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwa usalama wao.
Hatua ya kushindwa kwa waasi wa M23 inadaiwa itachochea uhasama uliopo kwa serikali ya Rwanda dhidi ya Tanzania ambao umepelekea Rwanda kushikiana na baadhi ya nchi za EAC katika kuitenga Tanzania katika mipango ya maendeleo ya EAC
No comments:
Post a Comment