Wednesday, August 28, 2013

SIMBA, AZAM ZAIBUKA KIDEDEA, YANGA YABANWA MBAVU NA COASTAL UNION

Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akipiga shuti huku beki wa Coastal, Juma Nyoso, akijaribu kumdhibiti, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom  kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, imeendelea leo katika viwanja tofauti na mabingwa watetezi, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union, huku Simba SC wakiishinda JKT Oljoro 1-0 mjini Arusha wakati Azam FC wakishinda bao 2-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora.

Mbeya; Wenyeji Mbeya City wameshinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Mabao ya wenyeji yalifungwa na Paul Nonga dakika ya saba na Steven Mazanda dakika ya 90, wakati bao la Ruvu lilifungwa na Shaaban Suzan dakika ya 24. 

Tanga; Bao pekee la Fully Maganga dakika ya 62, lilitosha kuipa Mgambo JKT ushindi wa 1-0 dhidi ya Ashanti United kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Chamazi; Kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Dar es Salaam, JKT Ruvu iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Prisons 3-0. Mabao ya JKT yalifungwa na Machaku Salum dakika ya 44, Emmanuel Swita dakika ya 69 na Hussein Bunu dakika ya 87


No comments:

Post a Comment