“ Nafikiri ni wakati muhimu kuanzisha madarasa maalum ya saikolojia, ili kuwaweka sawa wanavyuo. Nasema hivyo kwa sababu uamuzi wa kujiua ni sehemu ya maradhi ya akili,’’anaeleza
Waandishi Peltzer Karl na Paswana Nancy katika
kitabu chao, Suicidal behaviour among South African university
students: Contributing factors, resources and prevention, (Sababu na
namna ya kuzuia vifo vya kujiua kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika
Kusini), wanataja sababu zinazochangia matukio ya kujiua kwa wanafunzi
hususan wa vyuo vikuu vya Afrika Kusini, ikiwamo ugumu wa masomo na
masuala ya kijamii.
Sababu nyingine ni ukosefu wa fedha, matatizo ya
kifamilia, imani za kishirikina, kubakwa, kuwa waathirika wa virusi vya
Ukimwi, kufiwa na ndugu na jamaa, na tabia binafsi.
Aidha, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Afya (WHO), zaidi ya asilimia 90 ya vifo vya kujiua
duniani vinatokana na matatizo ya akili kama vile kuwa na msongo wa
mawazo, unywaji pombe uliopitiliza na skizofrenia (magonjwa ya akili)
Ufumbuzi wa tatizo
Taarifa nyingi zinaonyesha wanafunzi wa vyuo
vikuu katika maeneo mbalimbali ni moja ya makundi mwathirika wa matukio
ya kujiua. Bila shaka elimu, hamasa na misaada mbalimbali inatakiwa
kutolewa vyuoni ili kulinda kundi hili muhimu katika jamii.
Huduma za ushauri hasa masuala ya kisaikolojia
vyuoni hazina budi kuanzishwa, kuimairishwa na kuwa rafiki ili kuvutia
idadi kubwa ya wanafunzi wanaokabiliwa na matatizo husika.
No comments:
Post a Comment