Monday, May 12, 2014

TUNAPASWA KUFUNGA MILANGO YA UCHOCHORO KIGOMA ILI KUNUSURU WIZI NA UBADHILIVU UNAORUDISHA NYUMA KIGOMA


By Butije H. 
"Fedha za miradi ya maendeleo Tsh 10,000. Fedha za matumizi ya kawaida Tsh 100,000" Kwa bajeti hii ya kutengwa kwa kiwango kikubwa cha fedha kwenye matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kutengewa fedha kiduchu hatutafika.
Ajabu ya kuogofya hapa ni kuengwa kwa bajeti halafu fedha inayopelekwa na serikali haifiki hata 50% ya fedha iliyotengwa na ile iliyopelekwa kutumika zaidi ktk matumizi ya kawaida na si miradi ya maendeleo.
Miaka kadhaa halmashauri nyingi zimekuwa zikipata hati chafu baada ya ukaguzi CAG lakini hakuna hatua za kinidhamu wala kisheria zinazochukuliwa kwa walihusika na kuchafua halmashauri hizo.
Nchi hii inaliwa na watawala tunahitaji kuwa na viongozi. Kila mwaka ambao wananchi wanapata fursa ya kuchagua viongozi wanajikuta wanapewa kitu kidogo na watawala na hatimae kuwarejesha watawala madarakani.
Msiba mkubwa ni pale anapokuja mtawala na sura iliyo na bashasha na sura ya kinafiki ya kukujali sana anakwambia naomba kura yako laikini chukua na hii (BUKU) itakusaidia kwa leo. Then hakuna zahanati anayojenga halafu mke wako anapotaka kujifungua zahanati inapatikana mbali unaomba mchango (20,000) kwa rafiki zako ukodi TAX umpeleke mkeo kituo cha afya kilichopo mbali ukajifungue.
Utamsikia mtawala huyo anakwambia ukinichagua nitashughulika nihakikisha shule ya chekechea hapa mtaani inakuwa na madawati lakini chukua hii (BUKU) itakusaidia leo. Anatoa buku hizo kwa watu zaidi na zaidi na zaidi fedha ambazo angeweza kununua madawati ya kutosheleza shule zaidi 100.
Hivi kweli huyu mzee wa BUKU analengo la kutatua tatizo la madawati au analengo la kutufanya tuendelee kukaa chini na kukosa ari ya masomo ili tufeli nae aendelee kututawala badala ya kutongoza?
Mwaka 2005 & 2010 neno BUKU, BUKU MBILI, BUKU TANO na HATA BUKU ZAIDI ilikuwa ndio wimbo wa njini huku ahadi lukuki zikitolewa na moja ya hadi hiyo ni kumaliza tatizo ln "NITAHAKIKISHA MABOMBA YOTE YANATOA MAJI, NAJUA SHIDA NA ADHA MUIPATAYO WANANCHI WA KIGOMA, SASA NASEMA SASA BASI, NATAMBUA TUNAKOSA MAJI BILA SABABU YOYOTE WAKATI TUNAZIWA TANGANYIKA AMBALO TUNAWEZ KUPELEKA MAJI YA BOMBA HATA TABORA"
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 nilipata faraja kuwa huwenda tatizo la maji likawa historia ndani ya manispaa ya Kigoma/Ujiji nikiamni kuwa tunawapinzani wanaotetea maslahi ya wananchi na tunawatawala wanaotaka kuonesha kuwa wao sio watawala bali ni viongozi wanaosikiliza kilio cha wananchi.
Mbunge wa CCM ambae anatoka katika chama chenye dola atahakikisha udola na mamlaka walonayo wanamaliza ukame na kutu zinazoendelea kutafuna mabomba yetu ambayo kutu hizo zinaweza kutusababishia maradhi mbalimbali kwa miaka michache ijayo kwa kutumia maji ambayo yanapatikana kama ngekewa.
Kwa upande mwingine halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeshikwa na upinzani huku wakijivunia kwa kuwa na meya kijana lakini nao wameshindwa kutatua adha wanayoipata mama, dada, kaka na ndugu zetu wote walioko Kigoma.
Hivi kigoma kunanini? Hapa mchawi anaeturoga tusiendelee ni nani? Ni wazi kuwa rasilimali na utajiri ulioko mkoani kwetu ndo mchawi wetu. Mwabwanyenye wanaharibu na kufunga kila mlango wa mpango wa kuendeleza mkoa wa Kigoma. ili wafungue mlango wa uchochoro na kutorosha na kutumia rasilimali za kigoma kwa maslahi yao.
Hao mabwanyenye wanajaribu hata kuandaa watawala na si viongozi ili wakatetee na kuendelea kufungua milango ya uchochoroni kwa maslahi yao binafsi.
Hivyo BACK TO KIGOMA MOVEMENT ni muhimu ili kwenda kufunga milango yote ya uchochoroni ili kufungua milango ya barabarani ambayo itakuwa na tija na neema kwa wanakigoma wote.
Wakazi wa KIGOMA vijana wenu wanaona uonevu katika mkoa wetu basi. Ni wakati wa kurejesha hadhi ya mkoa wetu.
Mungu ibariki LWAMA
Mungu wabariki WANALWAMA

No comments:

Post a Comment