Tuesday, February 26, 2013

MWANAFUNZI WA CHUO CHA SAUT AJINYONGA NA KUPOTEZA MAISHA


Mwanafunzi Athanas Ernest wa chuo cha SAUT amejinyonga na kupoteza maisha leo asubuhi katika eneo la Malimbe .jijini Mwanza huku sababu za kujinyonga kwake zikiwa bado hazijafahamika.

Mganga wa Chuoni hapo  DR. Mnema amthibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo marehemu alijinyonga kwa kamba aliyoifunga kwenye kenchi ya dari chumbani kwake.
Marehem Athanas alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Sanaa na Elimu (Bachelor of Arts with Education) na alikuwa akiishi na mwanafunzi ambae alikuwepo eneo la tukio na jina lake halikuweza kutambulika mara moja kutokana na hali ya mazingira iliyokuwepo wakati huo.

Akikzungumza na Tanganyika One DR. Mnema amesema tukio hili ni la kusikitisha kwani hakuna aliyeamini kijana huyu msomi angeweza kufanya kitendo cha kujinyonga.
Tanganyika One ilipotaka kujua ni sababu zipi zilizopelekea kujinynga kwake, DR. Mnema alibainisha kuwa ni mapema mno kuzijua kwani hakuna maandishi yaliyoachwa na marehemu bali uatafanyika uchunguzi ili kubaini sababu zilizopelekea tukio hilo.

Kufuatia tukio hilo watu wametakiwa kuwa wawazi pingi wanapokabiliwa na matatizo ili waweze kusaidiwa. " watu wawe wawazi pindi wanapokabiliwa na msongo wa mawazo na matatizo ili waweze kupata msaada na kuepukana na vitendo kama hiv" alisema DR. Mnema huku akibainisha kuwa watu huwa wanachukua uamuzi kama huu ili kuepukana na matatizo yanayowasonga wakiamini kuwa kuko waendako wanakwenda kupumzika na hakutakuwa na matatizo kama yanayowakabili hapa duniani.

" Huenda huko kuna matatizo na shida kubwa kuliko zilizoko hapa duniani hivyo si vyema watu kuchukua uamuzi wa kujipeleka huko kabla ya wakati uliopangwa na Mungu. Alisema DR. Mnema  akiwaasa watu wasichukue uamuzi kama huo wakiamini watakwenda kupumzika matatizo yaliyoko duniani.

Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi.

Marehemu Athanas alikuwa ni mkazi wa Mpanda mkoani Katavi.

Mwandishi: Butije H.

No comments:

Post a Comment