Sunday, September 29, 2013

HATA YESU ALITUMIA "Twetter"


 

VATICAN CITY, Vatican

KANISA Katoliki limesema Yesu Kristu ndiye muasisi wa mawasiliano ya mtandao wa kijamii ‘tweeter’ kupitia katika mafundisho aliyotoa kwa wafuasi wake.
Askofu Mkuu wa Vatican, Mwadhama Gianfranco Kardinali Ravasi (pichani) alibainisha hayo ambapo alisema kwa vile mafundisho ya Yesu yalikuwa ni mafupi na yenye ujumbe ni sawa na mtandao huo.
Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano alisema Yesu alitumia tweeter kabla ya mtu yeyote kuanza kufanya hivyo kwani alitumia maneno chini ya 45 na yalieleweka.
Kardinali Ravasi alitolea mfano moja ya mafundisho aliyotoa yakiwemo ‘Mpendane’ ambapo alisema ingawa ni neno moja, limetoa ujumbe mzito kwa watu.

Katika kuonesha kuwa mitandao ya kijamii kama tweeter ni muhimu, kanisa hilo limeanza kuitumia ambapo kiongozi wake duniani, Papa Francis huutumia kuwasiliana na wamini.
Kasisi huyo alisema ni muhimu pia kwa makasisi wengine kutumia mitandao katika kulifikisha neno la Mungu kama anavyofanya Baba Mtakatifu kwazaidi ya waamini milioni 3 anaowasiliana nao.
“Kama kasisi au mhubiri hatumii njia za mawasiliano, atakuwa hatimizi wajibu wake inavyotakiwa kwa watu anaowaongoza au kuwafundisha.
CAHANZO: JAMBO LEO

No comments:

Post a Comment