Friday, September 13, 2013

TANGANYIKA ONE YAMPONGEZA KIPANYA KWA KAZI ZAKE ZINAZO AKISI JAMII YETU.






Blog ya Tanganyika One inampongeza mchora katuni wa Mwananchi Communication LTD Bw. Masud Kipanya kwa kazi yake ya uchoraji katuni zinazoonesha hali halisi ya masuala mbalimbali yanayotokea katika jamii yetu.

Kipanya amekuwa akitumia kalamu yake kuonyesha dhuluma inayofanywa kwa wananchi wa tabaka la chini na hali ngumu ya maisha ya watanzania.
TANGANYIKA ONE imeamua kumpongeza kwani kupitia kazi zake viongozi wa serikali, vyama na taasisi za kijamii wanaweza kujitazama kwenye kioo cha Bw. kipanya na kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

ALLAH ibariki Afrika, ibariki Tanzania na Umbariki Masud Kipanya.

No comments:

Post a Comment