Thursday, September 26, 2013

MAKAO MAKUU YA UN YAONDOLEWE MAREKANI



Rais Evo Morales wa Bolivia amesema kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuondolewa New York Marekani na kupelekwa katika nchi nyingine kutokana na siasa za Washington za kutoa vitisho na kutumia mabavu dhidi ya nchi nyingine.

Rais wa Bolivia ambaye alikuwa akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesisitiza kuwa makao makuu ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kuwa katika nchi inayoheshimu sheria na makubaliano yote ya kimataifa na isiyotoa hifadhi kwa magaidi na kuwalinda mafisadi. 
Morales amelaani hatua ya Marekani ya kumzuia Rais wa Venezuela kuhudhuria mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York na kuongeza kuwa, 

"haiwezekani kwa mtu asiyeamini ubeberu na mfumo wa kibepari kuwa na usalama mjini New York" alisema Morales.
Morales vilevile amemkosoa vikali Rais Barack Obama wa Marekani na kusema: Obama hawezi kuzungumzia amani na uadilifu wakati nchi yake inaendelea kuingilia masuala ya nchi nyingine na kufanya dhulma katika nchi hizo.

No comments:

Post a Comment