ZAIDI ya Watoto 97,000 Mkoani Kigoma wamepatiwa chanjo aina ya (PCV-13) dhidi ya magonjwa Hatarishi ya kuhara kukali,enomonia na uti wa mgongo ambao husababisha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Kauli
hiyo ilitolewa leo Kwenye kituo cha Afya cha Gungu Kigoma Ujiji ,ikiwa
na tija ya kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kutoka 99% kwa mujibu wa takwimu ya 2004 ya (Tanzania DemographicHealth Survey) ili ifikapo
2015 iwe 90% ya vifo hivyo visiwepo, hali ambayo iliwashawishi wananchi
kuitumia fursa hiyo kikamilifu ambapo watoto 97 ,000, walifanikisha
zoezi hilo la chanjo dhidi ya magonjwa korofi ikiwemo kichomi, uti wa
mgongo sanjari na kuhara kukali ambapo kunachochea kufariki kwa watoto hao.
Akizindua
chanjo hiyo Mkuu wa Mkoa Kigoma Lt.Issa Machibya alisema lengo la
kuzindua utoaji wa chanjo hizo ni pamoja na kupiga hatua za kutokomeza
vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, kutokana na magonjwa ya
kuhara na enomonia hali inayohatarisha kizazi cha leo na cha kesho
katika mkoa wa Kigoma na kitaifa.
Machibya amesema anaipongeza serikali na wataalamu wa afya kwa kuthibitisha kuwa chanjo aina ya`PNEUMOCOCCAL(PCV13) kuwa ni salama hukinga nimonia kwa 38% na uti wa mgongo zaidi ya 87% ,alafu jamii hailipii ni
bure , pelekeni watoto waepukane na adha ya magonjwa hatarishi
msisikilize wazushi eti msiwapeke hawawatakii mema vijana wetu.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Leonard Subi amesema kuwa,2009 chanjo zilikuwa zikitolewa dhidi ya magonjwa nane lakini leo chanjo hutolewa dhidi ya magonjwa 11 baada
ya kuongezeka chanjo mpya 2(PCV-13) ambazo zinakidhi kudhibiti maradhi
hatarishi ya kuhala kukali,kichomi na uti wa mgongo
CHANZO: Magreth Magosso,Kigoma
No comments:
Post a Comment