Na Magreth Magosso,Kigoma
Shirika la Reli Tanzania Kituo cha Kigoma,imeshindwa kudhibiti mtandao wa kuhujumu mapato yake kwa kuogopa mtandao wa uchawi.
Kauli hiyo imejitokeza
Kigoma ambapo Naibu waziri wa uchukuzi Mh,Charles Tizeba alipolitembelea
shirika hilo kukagua utaratibu wa uongozi huo kwenye usafirishaji wa
abiria na mizigo ambao ulikuwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo viongozi
kutumiwa na mtandao huo wa uchawi ambao huwaroga baadhi ya viongozi wao .
Fanuel Rugonzibwa ambaye ni
Mkuu wa Kituo hicho alisema ,mtandao huo unachangiwa na viongozi
walioko juu kuwapa jeuri ya kufanya jambo lolote bila kufuata sheria na
taratibu za kazi kuwategemea waganga wao,kwa watakaokiuka matakwa yao.
Alidai,kutokana na hali
tete ya kukithiri mtandao huo ambao hudiriki hata kuvujisha siri ya
vikao vya utawala na kwa viongozi ambao wanamsimamo wa kutetea haki na
stahiki za abiria ambao wanateseka na kudhulumiwa haki za msingi ikiwemo
kuuziwa tiketi juu zaidi ya kiwango cha serikali cha sh.19.100.
Akichangia katika hilo
Askari Polisi wa Reli mkoani hapa Koplo.Michael amedadavua kuwa,mtandao
huo unaongozwa na vijana wawili Said Ngururka na Majaliwa Zuberi
wamekuwa wakifanya hujuma hizo za kuuza tiketi zaidi ya bei husika na
kuvujisha siri za kituo hicho na kutoa taarifa za uongo kwa uongozi wa
juu ambapo huwachukulia sheria wafanyakazi wake bila kufanya uchunguzi
wa kina.
Akijibu tuhuma hizo Mh,Dkt
Tizeba amemtaka mkuu wa kitengo cha polisi cha reli kuwa,atakapopata
taarifa ya wababe hao kuzengea maeneo ya kituo hicho siku za kusafirisha
abiria watiwe nguvuni ili wachukuliwe hatua za kisheria na kufikishwa
mahakaman sanjari na sheria kuchukua mkondo wake, ili iwe fundisho kwa
wale wote wanahujumu shirika hilo.
" mtandao wa kichawi
utafanyiwa kazi,pia wafanyakazi wa reli muone uchungu na shirika
hili,acheni udokozi wa fedha za abiria wasio na tiketi na kugawana fedha
za mizigo ambayo haikubainishwa katika kitabu cha risiti "alisema
Tizeba.
Naye mkuu wa wilaya Kigoma
Ramadhani Maneno amewashauri watendaji wa shirika hilo wajitume kwa
dhati ili kuwaunga mkono waziri wa uchukuzi Mh,Harrison Mwakyembe na
Naibu wake Dkt.Tizeba ikiwa na tija ya kuwarudishia imani wananchi wake
,kwa kuwaondolea adha ya urasimu wa upataji wa tiketi na gharama za
usumbufu wa ughahirishaji wa safari hasa waishio mbali na manispaa ya
Kigoma Ujiji.
UPUUZI UPUUZI UPUUZI UPUUZI UPUUZI UPUUZI HAKUNA POINT HAPA
ReplyDeleteHUWEZI KUMJUA MCHAWI KAMA WEWE MWENYEWE SI MCHAWI. UCHAWI HAUWEZI KUMSHIKA MTU MPAKA NAYE AWE AMEJIHAMI, HUYO ANAYEAMINI UCHAWI NAYE UJUE KAJIHAMI SANA NDO MAANA ANAWAJUA WACHAWI. HABARI HII HAIFAI HATA KUCHAPISHWA NA MUUNGWANA.
ReplyDelete