Tuesday, January 22, 2013

POLISI MWANZA WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUTAWANYA MAANDAMANO YA WAENDESHA BODABODA

Jeshi Polisimkoani Mwanza limelazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwadhibiti waendesha pikipiki maarufu (Bodaboda) waliokuwa wakiandamana kama ishara ya kufikisha kilio chao dhidi ya manyanyaso wayapatayo toka kwa askari wa usalama barabarani na kushinikiza kuachiwa kwa wenzao waliokamatwa mapema hii leo.
Waendesha bodaboda hao waliandamana kupinga hatua ya Askari wa Jeshi hilo kuwasaka wenzao na kuwakamata kwa madai kwamba hawana Leseni ya kuendesha bodaboda na ya kufanya biashara ya kubeba abiria.
Akizungmza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Mwanza amesema jeshi la polisi liko katika msako mkali wa kuwakamata waendesha bodaboda ambao wanakiuka sheria za usalama barabarni kama kuendesha pikipiki bila leseni, kufanya biashara ya kubeba abiria bila leseni ya biashara, kubeba abiria zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja (mishikaki)
Kamanda amesema waendesha bodaboda wamekuwa wakikiuka sheria za barabarani pamoja na kuwagonga watembea kwa miguu na kukimbia bila kutoa msaada wowote kwa mwathirika.

No comments:

Post a Comment