Mpango wa Ujenzi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam leo umesababisha hasara kubwa kufuatia kuanguka kwa ukuta wa ndani kwenye maegesho ya magari madogo.
Baada ya ukuta huo kuanguka magari pamoja na baadhi ya watu wameweza kujeruhiwa, hata hivyo jitihada za makusudi za kupunguza uharibifu zinaendelea.
"nipo hapa tokea alfajiri nilikuwa namsindikiza mgeni wadngu, ghafla nikasikia kishindo kikubwa kutahamaki watu wakaanza kukimbilia eneo la tukio nilipofika hapa nikakuta kumbe ukuta huu eneo la maegesho ya magari madogo umebomoka" alisema mmoja wa mashuhuda ambae hakutaka jina lake libainishwe.
Aidha taarifa za awali zimeeleza kuwa huenda kukawa na watu waliokufa kwani baadhi ya watu hupenda kukaa katika eneo hilo wakisubiri kufanyika kwa biashara mbalmbali.Ingawa pia zimeeleza kuwa majeruhi wa tukio hilo wamekimbizwa katika kituo cha afya cha Palestina kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Aidha watu wamehoji kwa nini wahusika wa ujenzi huo waanze kuvunja kuta hizo alfajiri wakati wanajua kuwa kunakuwa na pilikapilika nyingi, pamoja na hayo jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa suala hilo.
No comments:
Post a Comment