Wednesday, January 23, 2013

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA AKALIA KUTI KAVU

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Willson Kabwe
Chama cha Mapinduzi kiko katika mkakati wa kumng'oa madarakani Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe kwa madai kuwa amechangia maendeleo  mabaya ya Chama hicho jijini Mwanza.
Mkurugenzi huyo anatuhumiwa na CCM kuhusika katika utapeli wa Sh1.6 bilioni za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akibainisha suala hilo Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde amesema,  amelifikisha suala hilo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula, akidai kuwa tuhuma hizo zilichangia CCM kupoteza ushindi katika uchaguzi mkuu.
Taarifa za ndani ya kutoka CCM zinadai kuwa Mbunge huyo na wenzake pamoja na Makamu Mwenyekiti huyo walikutana katika Hoteli ya New Mwanza na kujadili masuala mbalimbali na kufikia maamuzi kuwa CCM lazima ibadili hali ya siasa katika Jiji hilo huku wakiahapa kwamba ili wafanikwe kisiasa katika eno hilo ni lazima Mkurugenzi huyo afukuzwe kazi.
"Nikweli kwamba hali ya kisiasa jijini Mwanza siyo nzuri na anayesababisha hayo yote ni Mkurugenzi huyo, ingawa sisi nhatuna mamlaka ya kuamua suala lake ndiyo maana tumeamua kufikisha suala lake katika ngazi husika,ila hatukulifisha kama kesi isipokuwa kama taarifa ya kawaida ama mazungumzo"alisema Lusinde.

No comments:

Post a Comment