Thursday, January 17, 2013

JK amaliza mgogoro Madagascar


RAIS wa Serikali ya Mpito ya Madagascar, Andry Rajoelina ametangaza kutowania tena katika uchaguzi wa urais wa nchi hiyo unaotarajia kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Uamuzi wa kutogombea tena nafasi hiyo ulitangazwa jana na Rais Jakaya Kikwete mbele ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Benin, Beni Yayi Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mazunguzo baina yao.
Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ulinzi na Usalama ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc)- Troika, awali alikutana na mpinzani mkuu wa Rais Rajoelina ambaye ni Rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana na kumshawishi kukukubali kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni nchini Afrika Kusini tangu mwaka 2009
Pia Rais huyo alitangaza kukubali kutokugombea tena ili kuleta amani na utulivu. “Nimezungumza na Rais Rajoelina na amekubali kutogombea uchaguzi ujao kama uamuzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya hivi karibuni,” alisema.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete, Rais Rajoelina ametangaza rasmi uamuzi huo juzi nchini kwake na kwamba sasa uchaguzi huo utakuwa wa kidemokrasia na utasimamiwa na Umoja wa Afrika (AU) ambapo marais wote wanatakiwa kuheshimu makubaliano ya umoja huo. Awali, Rais Kikwete alisema kuwa migogoro mingi ya Afrika inasababishwa na wanasiasa ambao wanatumiwa na nchi zilizoendelea kwa masilahi yao.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment