Kufuatia sakata la Gesi Mtwara kuwa mgogoro kuhusu gesi unachochewa na wanasiasa kwa lengo la kukwamisha juhudi za Serikali za kumaliza tatizo la mgawo wa umeme, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema huo ni uzushi. Katika taarifa yake , Zito amesema Serikali haitashinda vita hii kwa kuzusha kwamba wanasiasa wanaopinga wanatumika na kampuni nyingine au kwa mataifa ya magharibi kutaka kuvuruga nchi.
“Serikali ijitazame yenyewe. Bila kufanya hayo
tunayo pendekeza, wananchi wataendelea kupigania haki yao...Hii ni vita
ya uwajibikaji. Wananchi wanataka kufaidika na rasilimali za nchi yao.
Kwa mujibu wa Zitto, Serikali imekuwa ikitoa
majibu ya porojo na kuwatusi watu wa Mtwara, na kama ilivyozoeleka Rais
Kikwete na mawaziri wake wamekuwa wakisema suala la Mtwara linatumika na
wanasiasa kujitafutia umaarufu.
“Inasikitisha sana kuona Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akiwaambia mabalozi wa nchi za kigeni waliopo hapa
nchini kuwa yanayoendelea mkoani Mtwara yanachochewa na wanasiasa
tuliosimama na wananchi wanaodai kufaidi utajiri wa nchi yetu. Rais
Kikwete na mawaziri wake wameshindwa kabisa kuonyesha uongozi katika
suala hili na hatimaye kuhatarisha umoja wa kitaifa.”
Aliongeza kuwa anafahamu kwamba Ubalozi wa China
umeandika barua serikalini kuwaondoa raia wa China waliopo Mtwara kwa
hofu ya maisha yao. Serikali inaficha ukweli huu kama ilivyoficha ukweli
kwamba Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
alifukuzwa na wananchi alipokwenda huko hivi majuzi. Serikali itaficha
ukweli mpaka lini?” alihoji.
SIMBACHAWENE
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesisitiza kuwa mgogoro na vurugu zinazoendelea mkoani Mtwara kuhusu gesi unachangiwa na wanasiasa.
Alisema kuwa watu hao aliodai wanakosa uzalendo na
utaifa, wanalenga kuhakikisha tatizo la umeme linaendelea kuwepo nchini
hadi uchaguzi mkuu ujao ili wapate ajenda ya kisiasa jukwaani.
No comments:
Post a Comment