Sunday, March 10, 2013

MWANAFUNZI AUA WATU WA 3 NA KUMI MAHUTUTI

 Na Magreth Magosso,Kigoma

Polisi Mkoa wa Kigoma linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha sita  Stanford Richard (30) mkazi wa kijiji cha Bitale wilayani humo, kwa  kufanya mauwaji ya watu watatu na kujeruhi kumi  ambapo majeruhi nane wako mahututi katika hospitali ya Mkoa  Maweni .
Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa Dismas Gapikakisusi  kigoma ujiji jana  alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari juu ya tukio hilo ambalo ni janga  kwa kijiji cha Bitale na mkoa mzima.
Gapikakisusi alibainisha kuwa, chanzo cha mauwaji hayo  ni sintofahamu, ingawa kijana huyo inasadikiwa baada ya kumaliza masomo yake sekondari kijiji hapo, alianza kuingiwa na hali ya kurukwa na akili na hadi jana kufanya mauwaji ya  Sebastian Julius(22) Rudia Richard (71) n,Ezema Lazaro(65)nyakati za asubuh.
" majeruhi wapo nane na hali zao ni mbaya hapo maweni ni pamoja na Pendo Jumbe(35),Jumbe Budio(50),Richard Manase(60),Rith James(55) na wengine watano huku majeruhi wawili wamepatiwa matibabu na wamerejea majumbani hamuwezi kumuona huyo kijana kwani hali yake ni tete" alidai Gapikakisusi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho alisema kuwa kijna huyo alianza kuwakata mapanga baba na mama yake kisha kuhamia myumba ya jirani kwa Jumbe Budio na kuishambulia familia yake  kwa kuwajeruhi kwa kutumia dive la gari na kipande cha nondo chenye mm 18  akiwemo mtoto wa shule ya msingi na kuhamia mtaani kuendeleza mashambulizi .
Baadhi ya majeruhi Pendo Jumbe na Dotto Issa wakiugulia maumivu makali huku wakiongea kwa kujivutavuta walibainisha kwamba,walishtukizwa na kipigo cha kitu kizito sehemu za kichwa hali iliyowapoteza fahamu na kujikuta wapo hospitali huku mama wa kijana huyo akiri kijana wake huwezi kuamini kama ni chizi kutokana na ukimya wake.
Mganga Mkuu wa Mkoa Leonard Sub akiri kuwepo kwa maiti hizo na majeruhi wakati  mkazi wa bitale  Aziza alipoulizwa juu ya tukio hilo alidai kuwa, ilikuwa saa moja za magharibi ndipo walisikia kelele za jamii kuwa  watu watatu walikufa  kwa kukatwakatwa na mapanga na wengine kujeruhiwa sehemu za kichwani  huku akidai kijana huyo ana tatizo la akili  baada ya kumaliza  kidato cha  sita kwenye moja ya shule za kata  kijijini hapo.

No comments:

Post a Comment