,Na Magreth Magosso,Kigoma,
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya `AMITIER’ iliyopo katika kambi
ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma,wanasadikiwa kufanya
mauwaji ya Tona Kabwe(63) kwa kumtuhumu kuwa ni mchawi. na walimu wao
wanne wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani hapo.
Taarifa hiyo imetolewa na ACP Frasser Kashai alipokuwa akizungumza
na wandishi wa habari ofisini kwakwe Kigoma Ujiji jana, alisema
22,Januari,2013 saa 4.20 kwenye kambi ya wakimbizi ya nyarugusu
wanafunzi hao wakiwa pamoja na walimu wao,walikwenda nyumbani kwa
marehemu kwa tija ya kutoa pole baada ya kufiwa na mjukuu wake ambaye ni
mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.
"inasemekana wanafunzi hao awali mjukuu wa marehemu ambaye naye
alifariki baada ya kuugua kwa siku chache hivi karibuni ,inasadikiwa
kabla ya kifo chache aliwahadithia baadhi ya wanafunzi wenzie juu ya
ndoto yake aliyomuota babu yake akimrisha nyama hali iliyowajengea imani
wanafunzi hao kwenda kulipiza kisasi kwa babu huyo kwa kumpiga na fimbo
sanjari na kuni hadi umauti ulipomfika" alisema Kashai.
Alidai kutokana na tukio hilo Jeshi la polisi linawashikilia walimu
wane wa shule hiyo kwa upelelezi ,huku akitoa rai kwa wananchi
wapunguze imani za kishirikina.Wakatihuohuo 22,Januari,2013,saa 10 jioni
kijiji cha kwaga wilayani kasulu watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni mke
na mume Hakani (45) na Prisca William wamekufa baada ya kupigwa na radi
wakiwa shambani.
Muguzi wa zahanati ya Kwaga Leonard Haiki alipohojiwa na wandishi
uwepo wa taarifa hiyo,alikana kufa kwa Prisca huku akidai kufa riki kwa
mumewe Hakai, na kubainisha majeruhi watano ambapo watatu wamepelekwa
kituo cha afya cha Kasulu. Wakati huohuo kijiji cha Nyarugusu saa 4.00
mtoto Sharifu Rajabu (15) amekutwa amekufa baada ya kujinyonga kwa kamba
ya chandarua chumbani kwakwe .
Kashai alidai chanzo cha kujinyonga kwake ni kitendawili na upelelezi bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment