Na Magreth Magosso,Kigoma
Walimu wa shule za msingi wanaofundisha katika Manispaa ya Kigoma Ujiji,wanapigwa msasa wa siku saba ili kubaini stadi za matumizi ya muundo mpya wa ufundishaji wa muhamo wa ruhaza ambao utasaidia kudhibiti tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.
imeanza kuendesha semina ya mafunzo hayo, kwa walimu kutoka shule mbalimbali za manispaa hiyo ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wasiojua kusoma na kuandika.
Hata hivyo kwa upande wake Naibu Mkaguzi wa elimu katika manispaa ya Kigoma Ujiji, George Ngwila alisema kuwa zipo sababu mbalimbali ambazo zinachangia katika kuwafanya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kufaulu mitihani yao ya mwisho kutokana na ushirikiano duni baina ya walimu, wazazi na wanafunzi wenyewe.
Ngwila amedai siku saba za kupewa elimu hiyo itasaidia walimu hao marejeo ya nini wanachopaswa kufanya katika utendaji wao darasani hasa suala la kuangalia muundo wa kusoma, kuandika na kuhesabu ili kuondoa tatizo hilo.
Mwalim Domiciana Peter ambaye amefundisha shule mbalimbali za msingi katika manispaa hiyo kwa miaka mingi alidai kuwa, kubadilishwa kwa mitaala kumechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wanafunzi wamalize elimu ya msingi wakiwa hawajui kusoma na kuandika.
Amesema kuwa kwa mfumo wa sasa wa mitaala haina stadi zile za KKK na ufanyaji wa mitihani wa kuchagua unawapa nafasi baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kuweza kupenya na hatimaye kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.
Ikumbukwe kuwa,zaidi ya wanafunzi47 waliomaliza shule ya msingi katika shule za manispaa hiyo 2012 walikuwa hawajui kusoma,kuandika wala kuhesabu,ingawa jitihada zimeanza walimu kupewa njia yakinifu ili kukabiliana na changamoto hiyo,lidara ya elimu ipeleke walimu wao mafunzoni kila wabadilishapo mitaala.
No comments:
Post a Comment