v Aagaiza utaratibu ulokuepo kwa muda mrefu uendelee
mpaka kamati itakayoundwa ipate muafaka
v Ataka kamati ya viongozi wa madhehebu ya dini iundwe
haraka kupata muarobaini wa tatizo hili
By Butije Hamisi
Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Mizengo
pinda ameagiza utaratibu uliokuwepo kwa muda mrefu wa waislam kuchinja katika
machinjio ya umma uendelee mpaka hapo kamati inayoundwa ya maafikiano ya viongozi
wa madhehebu mbalimbali ya kiislam na kikristo itakapokaa na kupata ufumbuzi wa
mgogoro huo.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kikao cha viongozi
wa madhehebu ya kiislam na kikristo kilichofanyika katika ukumbi wa BOT jijini
Mwanza Pinda amesema serikali haiko tayari
kuona mgawanyiko baina ya watanzania kwa kuruhusu mabucha ya wakristo na
waislam kwani mgawanyiko hautoishia hapo utakwenda mbali zaidi katika Nyanja za
kijamii.
“ Jambo hili si la kisheria, ni jambo ambalo limeibuka kwa
maridhiano ya kuheshimiana madhehebu haya makubwa mawili kwa muda mrefu. ”
alisema Pinda na kuwataka viongozi wa dini kuendeleza utamaduni huu ili kujenga
amani, utulivu na mshikamano baina ya watanzania.
Waziri pinda amesema yapo "makandokando" yaliyojitokeza na
kutochukuliwa hatua haraka ndio yaliyoleta
kuchocheachochea fikra hizi nakufanywa kuwa ajenda mojawapo kati ya
ajenda za msingi.
Pinda amemuagiza mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh Evarist Ndikilo
kusimamia shughuli za kamati inayoundwa ili kufikia muafaka wa tatizo hili
haraka iwezekanavyo
Habari zilizoifikia Tanganyika One zinaeleza kuwa kamati
hiyo itakuwa na wajumbe ishirini, kumi wakiwa viongozi wa kiislam na wengine 10
viongozi wa kikristo.
Pinda ametahadharisha
kuwa mgawanyiko huu utaziathiri taasisi kama magereza, jeshini,bunge na taasisi
zingine za umma kwa kutenga nyama ya wakristo na nyama ya waislam na hivyo
kupelekea watu kujigawa kwa kila jambo kitendo ambacho kinahatarisha amani na
utulivu wa nchi yetu.
Katika kikao hicho vituo vya radio vya Kwaneema Fm na Radio Iman
na DVD zilizopo mitaani za Sh. Ilunga vimelalamikiwa kuchangia kukua kwa mgogoro
huu na mamlaka husika kushauriwa kuchukua hatua madhubuti ili kuzuia vyombo
hivyo kuendeleza chuki kwa watanzania.
Meshimiwa Pinda natarajiwa Kesho kwenda mkoani geita ikiwa
ni moja ya jitihada za serikali kutatua mgogoo huu.
Hivi karibuni waziri wa nchi Ofisi ya rais uratibu na mahusiano Mh Stevine Wasira aliagiza wakristo wanaruhusiwa kuchinja majumbani kwao na katika shughuli zao binafi na waislam waengdelee kuchinja kayika machinjio ya umaa.
Mdogo wangu, unajitahidi kutuhabarisha kupitia blog hii lakini nakuomba upunguze haraka ya ku-type ili makosa ya ki-maandishi yawe machache. Habari hii nairejea mara nyingi na nimeamua kuigawa kwa wafanyakazi wangu ili iwaongoze kutambua masimamo wa serikali ktk suala la uchinjaji lakini ina makosa lukuli. Tafadhali hariri kabla ya ku-post habari yoyote. then hukukumbuka kuripoti kilichojiri baada ya kamati ya watu 20 kuundwa.
ReplyDelete