- Rais Kikwete amtaka Uhusu Kenyatta aingie Ikulu kama Rais na si kama mtoto aliyekulia Ikulu ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa sababu kukulia Ikulu ni tofauti na kuishi kama Rais wa nchi.
Rais Uhuru Kenyatta akila
kiapo cha Urais,kuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,kwenye sherehe
zilizofana kwa kiasi kikubwa ndani ya uwanja wa kasalani.Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh
Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake,
mapema leo kwenye sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi
Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi mbalimbali
na watu mbalimbali.Picha zote kwa hisani ya Mike Kariuki wa Capital FM.
Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na Makamu wake
William Ruto.
Rais wa Uganda,Mh Yoweri Kaguta Museven akisoma
hotuba yake fupi wakati wa kuapishwa kwa Rais wa awamu ya nne nchini
Kenya,kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya uwanja wa Kasalani,jijini Nairobi.
Akizungumza baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo alisema kwamba suala la amani ya nchi hiyo ndiyo itakuwa ajenda ya kwanza katika utawala wake.
"Ndugu zangu wakenya, suala la amani ni suala muhimu sana, kulinda amani ya nchi ni ngumu kuliko kuzua vurugu mdani ya nchi,napenda kuwahakikishia kwamba amani itaendelea kutawala Kenya na kamwe sitapenda kuona mtu yoyote akijaribu kuivuruga amani yatu"alisema Rais Kenyatta.
Kuhusu suala la ajira nchini humo alisema,"Kazi ya pili itakayofuata ni kazi ya kuhakikisha kwamba watu wasiokuwa na ajira wanapata ajira ndani ya nchi kwani kwa kipindi kirefu wakenya wamekuwa wakikosa kazi huku wataalam mbalimbali wakitoka nje ya Kenya" , Kwa upande wake Makamu wa Rais William Ruto alisema kwamba huu ni muda wa kuwatumikia wakenya na hiyo ndiyo kazi iliyopo mbele yao.
Naye Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akitoa salamu kwa niaba ya viongozi mbalimbali walioalikwa katika sherehe hizo alimtaka Kenyatta aingie Ikulu kama Rais na si kama mtoto aliyekulia Ikulu ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa sababu kukulia Ikulu ni tofauti na kuishi kama Rais wa nchi, huku pia akimwakikishia ushirikiano mkubwa katika jumuia ya Afrika Mashariki.

No comments:
Post a Comment