Wednesday, April 17, 2013

TUNDU LISSU AZUA BALAA BUNGENI, TBC WAKATA MATANGAZO KUFICHA UKWELI


HALI imekuwa tete katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, Baada ya Naibu Spika Job Ndugai kuamuru askari wa bunge kumwondoa nje ya Ukumbi wa Bunge,  Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu.

Hata hivyo Lissu pamoja na baadhi ya wabunge wa Chadema walisikika wakisema kwamba, hatoki mtu hapa, huku Ndugai akiendelea kusisitiza kwamba ili bunge liendelee ni lazima Lissu atoke kwanza.
Sababu kubwa iliyomfanya Ndugai amfukuze Lissu bungeni inatokana na hatua ya Lisssu kutaka kuzungumza, huku Naibu Spika akidai kwamba Lissu amezungumza mara nyingi tofauti na taratibu za bunge hilo.
Hata hivyo hatua hiyo iliendelea kwa zaidi ya dakika 15 kiasi cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lililokuwa likirusha matangazo hayo moja kwa moja kukata matangazo yake kwa dakika tano.
Hata hivyo walijaribu kurudi hewani hali ikawa bado inaendelea ndipo TBC ilipoamua katisha matangazo hayo mpaka kesho ili kukwepa kuonya hali ya hatari iliyokuwa ikiendelea katika bunge hilo mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

SOURCE: Habarimpya.com

No comments:

Post a Comment