Saturday, December 15, 2012

MWALIM AKUTWA MTUPU SHULENI


MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.
CHANZO: MWANANCHI

20% YA BIDHA BIDHAA ZINAZOINGIA NCHINI NI FEKI


ASILIMIA 20 ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini ni bandia, hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kigoda alisema kama hali hiyo itaachwa iendelee itasababisha madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa jumla.
Alisema kuenea kwa soko la bidhaa bandia nchini kunatokana na bei za bidhaa hizo kuwa ndogo, hivyo kuwavutia wateja wengi.
“Watanzania wenye kipato cha chini ndiyo wapenzi zaidi wa bidhaa hizi lakini wanatakiwa kutambua kuwa madhara yake ni makubwa mno,” alisema Dk Kigoda na kueleza kuwa Serikali imetangaza vita na wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa hizo.
Dk Kigoda aliwataka wafanyabiashara wanaouza bidhaa hizo kuziondoa sokoni haraka kabla Serikali haijaanza kuziondoa kwa nguvu. Waziri Kigoda alisema uchunguzi umebaini kuwa, kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani, kuna bandari bubu 32, ambazo hutumika kupakua bidhaa hizo bandia.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni matairi ya magari na pikipiki, mafuta ya kupaka, maziwa ya watoto, nyaya za umeme, simu za mkononi na vyakula mbalimbali.
Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, wizara yake inashirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuchunguza bidhaa zinazoingia nchini kabla hazijasambazwa katika soko.
Alipoulizwa ni lini operesheni ya kuwakamata wanaouza bidhaa hizo itaanza, Dk Kigoda alimtupia swali hilo Katibu Mkuu wa Wizara yake, Joyce Mapunjo ambaye alisema huenda ikaanza leo, huku akisema wizara inachokifanya kwanza ni kutoa tahadhari. Dk Kigoda akaongeza... “Tukianza (operesheni maalumu) hatutakuwa na mjadala.”
“Zipo nyaya bandia za umeme ambazo kwa kiasi fulani zinaweza kuwa chanzo cha kuongezeka kwa matukio ya nyumba kuteketea kwa moto nchini, pia yapo matairi ya magari na pikipiki ambayo nayo kwa kiasi fulani yanachangia kuongezeka kwa ajali.”
Akitolea mfano Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Kigoda alisema kuanzia Januari mpaka Novemba mwaka huu, kulikuwa na ajali za pikipiki 1997, zilizosababisha vifo vya watu 140.
“Tumejipanga kuhakikisha jambo hili tunalimaliza kabisa, kwanza tumegundua bandari bubu 32 ambazo pamoja na mambo mengine, zinaifanya Serikali kukosa mapato na kuhatarisha usalama wa wananchi” alisema Dk Kigoda.
Alisema kuwa tayari wameshazieleza taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya kutumia bidhaa bandia yakiwamo ya hasara kutokana na kuharibika katika kipindi kifupi.
CHANZO: MWANANCHI

UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE HAUKUBALIKI

Mkuu wa idara ya mawasiliano ya umma (SAUT) Bi Imane Duwe (picha kubwa katikati)  akiwa ktk kongamano la  jinsia na afya ya uzazi lililoandaliwa na wanafunzi wa mawasiliano ya umma mwaka wa tatu SAUT lililofanyika katika ukumbi wa Mgulunde chuoni hapo.
moja ya sababu zinazowafanya wanawake wa kati ya umri wa miaka 17-25 watoe mimba kwa kuhofia kupoteza shepu ya maumbile yao. pia wamekuwa wakitoa mimba kuwa sababu ya kuwa na wapenzi wasio wa kudumu.
Tanzania inachukua nafasi ya tano duniani kwa wanawake kufanya kazi mbalimbali bila kupata malipo (ujira) kwa kazi mbalimbali wanazozifanya. Hayo yamesemwa na Bi Khadija Liganga (kulia) toka kivulini wakati akiwasilisha mada ktk kongamano la jinsia na afya ya uzazi lililoandaliwa na wanafunzi wa shahada ya mawasiliano ya umma mwaka wa tatu ktk chuo cha SAUT.

Thursday, December 13, 2012

UTOFAUTI WA KIPATO

Hivi bado tupo kwenye ujamaa? Tanzania nchi inayoamini kwenye ujamaa, lakini pengo la walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka.

Saturday, December 8, 2012

MIGONGO 1950: AJALI MBAYA TENA IRINGA 10 WATAJWA KUFARIKI, 42 MA...

MIGONGO 1950: AJALI MBAYA TENA IRINGA 10 WATAJWA KUFARIKI, 42 MA...: STORY YA http    ZIKIWA  zimepita  siku takribani  tatu  toka ajali mbaya  itokee katika kata ya Mseke katika...

MIGONGO 1950: AJALI MBAYA TENA IRINGA 10 WATAJWA KUFARIKI, 42 MA...

MIGONGO 1950: AJALI MBAYA TENA IRINGA 10 WATAJWA KUFARIKI, 42 MA...: STORY YA http    ZIKIWA  zimepita  siku takribani  tatu  toka ajali mbaya  itokee katika kata ya Mseke katika...
Matukio katika harambee ndogo ya kuchangia mfuko wa harambee kubwa itakayofanyika  reb, 2013 ya kupanua usikivu  wa radio IQRA FM- Mwanza

Matukio katika harambee ndogo ya kuchangia mfuko wa harambee kubwa itakayofanyika  reb, 2013 ya kupanua usikivu  wa radio IQRA FM- Mwanza

South Africa's Nelson Mandela in hospital 'for tests'


File picture taken on June 17, 2010 shows former Nelson Mandela at the funeral of his great-granddaughter in Sandton, north of Johannesburg
South Africa's former president Nelson Mandela has been admitted to hospital in the capital Pretoria to undergo tests, officials say.
The office of President Jacob Zuma said 94-year-old Mr Mandela was doing well and there was "no cause for alarm".
Mr Mandela spent more than two decades in jail under the white minority apartheid regime.
He served as South Africa's first black president between 1994 and 1999, and received the Nobel Peace Prize in 1993.

JUQUSUTA YAJIPANGA KUPANUA USIKIVU WA RADIO IQRA- Mwanza

toka kushoto, Shekh wa mkoa wa Mwanza Salum Fereji, Mlezi wa Samuko Artaf hiran,  M/kiti wa Mwinyibaraka Foundation Sh. Issa Othman, M/kiti wa JUQUSUTA taifa Sh. Hassan Kabeke na mwekahazina wa JUQUSUTA Mohammed Kassanga wakiwa katika harambee ndogo ya kupanua usikivu wa IQRA Fm radio. Harambee hiyo ni maadalizi ya harambee kubwa itakayofanyika february 2013.

Nguo za ndani zachangia ugumba


TAFITI za kisayansi zimebaini kuwa nguo za ndani hasa zinazobana kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa mbegu za kiume, hivyo kushindwa kutunga mimba.
Utafiti huo uliofanyika katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zilizotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba.
Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga ujauzito katika nyumba ya uzazi ya mwanamke.
Akizungumzia utafiti huo jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, alisema una ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.
“Kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” alisema Dk Massawe.

Ufaransa na Uingereza
Utafiti uliofanywa Ufaransa umebaini kuwa, upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi ulianza kutokea tangu mwanzoni mwa 1990.
Awali, ilikuwa ikiaminika kuwa kupungua kwa uwezo wa mbegu za kiume kulitokana na sababu kama vile mtindo wa maisha, ulaji na matumizi ya dawa kupindukia na matumizi ya vyakula vyenye kemikali nyingi, lakini safari hii utafiti umebaini kuwa matumizi ya nguo za ndani yamekuwa yakiwaathiri wanaume wengi.
Mtafiti wa Uingereza, Profesa Richard Sharpe anasema tatizo hilo linaweza kuepukwa ikiwa mhusika atajitahidi kuvaa nguo zinazokubalika na mahala alipo. Hata hivyo, anapendekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho.
Mtafiti huyo kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh anasema: “Uingereza suala hili halijawahi kuonekana wala kutiliwa mkazo na kuwa kipaumbele katika afya, labda kwa sababu ya wasiwasi kwamba sehemu za mwanamume zinatakiwa kubanwa. Hivi sasa hakuna shaka kwamba suala hilo ambalo liliongelewa hapo awali lina ukweli ndani yake, hivyo ni wakati kwa watu wote kuchukua hatua.
“Kutokuchukua hatua kutasababisha familia nyingi kukosa watoto na hivyo idadi ya watu itapungua, lakini katika hali ya kawaida, ni vyema watu wakaelimishwa namna ya uvaaji. Sehemu za joto mtu anatakiwa kuvaa pamba na si nailoni ili kulinda mbegu zake.”
Profesa Sharpe anasema bado wanasayansi wana kazi kubwa kwani mpaka sasa karibu kila eneo ambalo wanasayanasi wamelichunguza limebainisha kuchangia tatizo hilo, lakini mpaka sasa wanafikiri kuwa vyakula vyenye mafuta na vile vyenye kemikali nyingi vina mchango mkubwa zaidi katika tatizo hilo.
Watafiti ambao walitumia takwimu kutoka katika vituo vya afya 126, waligundua kuwa tangu mwaka 1989 mpaka 2005, kulikuwa upungufu wa uwezo wa manii kwa mwanamume kufanya kazi kwa asilimia 32.2, kiwango ambacho ni karibu asilimia mbili kwa mwaka.
Watafiti walisema: “Kwa ufahamu wetu, ni utafiti wa kwanza kufanyika na umehusisha mbegu za kiume hai na uwezo wa manii katika nchi nzima kwa kipindi kirefu.”
“Huu ni utafiti mkubwa na unatoa onyo kali kiafya kwa jamii. Lakini huwezi kumlazimisha mtu kuhusu matumizi ya nguo za ndani,” wanasema.
CHANZO: MWANANCHI

BAKWATA YACHANGIA UIMARISHAJI WA RADIO IQRA- MWANZA

Viongozi wa BAKWATA mkoa wa Mwanza wakiwa ktk hfla ya kuchangi utunishaji wa mfuko kuelekea harambee kubwa ya kuchangia upanuaji wa usikivu wa Radio IQRA FM. Radio Iqra ipo katika mkakati kabambe wa kupanua usikivu wake katika mikoa sita hapa nchini. kulia ni Shekh wa Mkoa wa Mwanza Sh. Salum Fereji na katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza Sh. Mohamed  S. Bala.

Tanzania kusimamia wanajeshi wa pamoja DRC


Jumla ya nchi kumi katika eneo la Maziwa makuu zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja litakalokuwa na jumla ya askari 4,000 katika kukabiliana na ghasia na vita vya mara kwa mara mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Waziri wa Ulinzi wa DR Congo, Dakta Crispus Kiyonga amethibitisha uundwaji wa jeshi hilo, akisema litafanya kazi chini ya usimamizi wa Tanzania.

Mapigano ya hivi sasa mashariki mwa Congo yalizuka mwezi Aprili mwaka huu wakati waasi wa M23 walipoliasi jeshi la nchi hiyo na kusababisha watu laki tano kuyakimbia makaazi yao wakihofia usalama wao.
Wakati huohuo, viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika, SADC, wameanza mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini Tanzania.
Wameanza kwa kufanya kikao cha Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe, kikao hicho cha TROIKA kimewakutanisha marais Jakaya Kikwete, Hifikepunye Phohamba wa Namibia na Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Amesema mara baada ya kikao hicho cha TROIKA viongozi hao watajumuika na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kimataifa wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, pamoja na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa sasa SADC.
Viongozi hao kwa pamoja watajadiliana kwa kina matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Zimbabwe ambapo watawasilisha mapendekezo yao katika mkutano mkuu wa viongozi wote 14 wa SADC utakaofanyika kesho.

CHANZO: Idhaa ya BBC

MLIPUKO WA BOM WAJERUHI WATU 10 NCHINI KENYA


http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/6595d83c54ff005f9781fab0904b75ac_XL.jpg


Polisi ya Kenya imetangaza kuwa, watu wasiopungua 10 wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea karibu na Msikiti mmoja huko Nairobi mji mkuu wa nchi hiyo. Baadhi ya duru nyingine za habari zinaeleza kuwa, watu watatu wameuawa kwenye mripuko huo. Polisi ya Kenya imeeleza kuwa, mripuko huo umetokea katika eneo la Eastleigh, eneo ambalo wakazi wake wengi ni Wakenya wenye asili ya Kisomali. Siku ya Jumatano iliyopita, mtu mmoja aliuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu pambizoni mwa barabara katika eneo hilohilo la Eastleigh. Hadi sasa hakuna mtu au kikundi chochote kilichotangaza kuhusika na milipuko hiyo.

CHANZO: Idhaa ya kiswahili ya tehran

Thursday, December 6, 2012

TANGANYIKA ONE: Walimu Wakimbia Shule kwa Kubakwa na Wanafunzi

TANGANYIKA ONE: Walimu Wakimbia Shule kwa Kubakwa na Wanafunzi: Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa WALIMU  wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa...

Walimu Wakimbia Shule kwa Kubakwa na Wanafunzi

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa

WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao. Habari zilizolifikia Mwananchi jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.
Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.
Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.
“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku. Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.
Mwalimu huyo alidai kuwa walimu wamekuwa wakitishiwa kuchomwa visu na nyumba zao kuchomwa moto, huku walimu wanne wa kike wakidhalilishwa kimapenzi kwa kupigwa mabusu na kutongozwa na wanafunzi.
“Wanafunzi wamefanya mtihani wa kidato cha pili chini ya ulinzi wa askari polisi wenye silaha kitu ambacho si cha kawaida,” aliongeza.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Ofisa Elimu Sekondari, Adnan Mwenda alisema asingependa kuzungumzia tatizo hilo kwa kuwa siyo msemaji. Akashauri atafutwe mkurugenzi wa wilaya… “Unaweza kuzungumza mambo mengine yakakuletea matatizo,” alisema Mwenda kabla ya kuelekeza atafutwe mkurugenzi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard Rwegasira alithibitisha walimu hao kuikimbia shule hiyo na kusema kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, itakutana hivi karibuni kujadili suala hilo.
“Ni kweli shule hiyo imetelekezwa, walimu wamekimbia na wanafunzi hawaendi shule. Tatizo tunalifahamu na Mkuu wa Wilaya anafanya jitihada mbalimbali kurekebisha tatizo hilo,’ alisema.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruaruke, Hemedi Mpullu pia alithibitisha walimu hao kuitelekeza shule hiyo na kusema Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu ameagiza kufanyika kwa kikao cha dharura ili kupatikana mwafaka kati ya walimu hao, wanafunzi na wazazi.
“Mbunge wa Kibiti, Abdul Marombwa amepanga pia kufanya mkutano hapa Ruaruke ili kutafuta mwafaka,” alisema Mpullu. Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT), Wilaya ya Rufiji, Manyama Lazaro alisema kuondoka kwa walimu hao, kumefanya shule hiyo ijifunge yenyewe, kwani wanafunzi nao sasa hawaendi shule.
“Wanafunzi wamefikia hatua ya kuwachora walimu wa kike wakifanya mapenzi na walimu wa kiume katika kuta za vyoo! Huu ni udhalilishaji mkubwa,” alisema.
Lazaro alieleza kuwa katika siku za hivi karibuni, wanafunzi hao walichoma moto nyumba tatu za walimu na Bodi ya Shule iliamua kuwa wanafunzi hao waitwe na wazazi wao ili walipe gharama za uharibifu.
CHANZO:-Gazeti Mwananchi

MAMBO BADO MAGUMU KILIMANJARO STARs- CECAFA


Timu ya taifa ya Tanzania bara (Taifa Stars) bado hali ni tete. Ikiwa ni dakika 58 bado iko nyuma kwa magoli mawili dhidi ya Uganda. Okwi na Sentongo ndio walioleta kilio Tanzania.

Mhhhhhhhhhhh!



Kipanya
By Kipanya

ASKARI 12 WAUAWA SOMALIA


Maafisa kutoka jimbo lililojitenga la Puntland nchini Somalia wamesema kuwa wanajeshi kumi na mbili wa serikali ya Somalia wameuwawa na kundi la wanamgambo wa kislaamu la Al shabaab katika eneo la milima ya Galgalo
Taarifa zinasema kulikuwa na mashambulizi mawili tofautio ambapo wanajeshi waliuawa katika eneo la milimani la Galgalo.
Kwa mujibu wa taarifa za kundi la Al shabaab waliwauawa zaidi ya wanajeshi 30 wa serikali kabla kutoweka katika milima hiyo.
Wapiganaji wengi wa Al Shabaab wameripotiwa kukimbilia eneo la Puntland katika miezi ya hivi karibuni huku jeshi la Somalia pamoja na wanajeshi wa Muungano wa Afrika kudhibiti Kusini mwa Somalia

285 WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA KIMBUNGA "BOPHA" NCHINI UFILIPINO


Watu zaidi ya 285 wanaripotiwa kupoteza maisha kufuatia Kimbunga Bopha kusini mwa Ufilipino.
 mamia ya watu wengine wameachwa bila makao kufuatia kimbunga hicho kikali katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.
Pwani ya Palawana katika eneo la Mindanao limeathiriwa vibaya na Kimbunga Bopha chenye upepo wenye kasi ya kilomita 120 hadi 150 kwa saa.
Waziri wa Mambo ya Ndani Ufilipino Manuel Roxas amesema zaidi ya watu 300 wametoweka kufuatia kimbunga hicho.
Uharibifu mkubwa unaokadiriwa kupindukia dola milioni 100 umeripotiwa katika sekta za kilimo na miundombinu katika jimbo la Compostela.
Ufilipino hukumbwa na vimbunga kila mwaka na aghalabu husababisha vifo na uharibifu mkubwa.

AJALI YA NDEGE YAUA 11 AFRIKA KUSINI


 watu 11 wamefariki dunia kufuatia ajali ya helikopta ya kijeshi, mashariki mwa Afrika kusini. habari zinasema kuwa waliofariki dunia ni madaktari wa rais mustaafu, Nelson Mandela. Helikopta hiyo ilikuwa imetokea Pretoria ikielekea Mthatha karibu na mji wa Qunu, nyumbani kwa Mzee Nelson Mandela. 

ZANZIBA YAPOTEZAAFA NAFASI YA KUCHEZA FAINALI YA CECAFA



Timu ya Taifa ya zanzibar ZANZIBAR HEROES imepoteza nafasi ya kucheza fainali ya kombe la CECAFA baada ya kfungwa na Kenya kwa njia ya matuta.
Awali tumu hizo zilitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na kwenda hatua ya matuta ambapo kenya ilibuka na ushindi kwa penalt 4 kwa 2.
ZAnziba inaubiri nafasi ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya atakaepoteza kati ya Uganda na Tanzania bara.

Wednesday, December 5, 2012

RAIS MURSI AREJEA IKULU




Rais Muhammad Mursi wa Misri leo amerejea kwenye ikulu yake mjini Cairo, licha ya maelefu ya waandamanaji waaopinga katiba mpya kuendelea kukusanyika mbele ya geti la ikulu hiyo. Morsi jana jioni alilazimika kuondoka katika ikulu hiyo iliyoko kaskazini mwa mji mkuu Cairo, baada ya maelfu ya wandamanaji kuizingira ikulu hiyo na kutokea vurugu kati yao na polisi. Ambapo watu 20 walijeruhiwa.

IRAN YAPATA TAARIFA ZA SIRI KWA NDEGE YA MAREKENI ILIYOKAMATWA


Jeshi la ulinzi la Ira limefanikiwa kuchomoa habari zote za siri katika ndege ya kijasusi isiyo na rubani (drone) ya Marekani aina ya ScanEagle iliyonaswa hivi karibuni na jeshi hilo katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Idara ya Habari ya IRGC imesema kuwa 'drone' hiyo mbali na kufanya ujasusi kuhusu masuala ya kijeshi pia ilikuwa na jukumu la kukusanya habari za shughuli za usafirishaji mafuta katika bandari za Iran.
 Siku ya Jumanne Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran Admeli Ali Fadavi alisema kuwa wataalamu wa jeshi hilo walifanikiwa kushusha chini na kuinasa ndege hiyo ya kijasusi ya Marekani ambayo ilikuwa imeingia katika anga ya Iran ikiongozwa kutoka mbali. Ikumbukwe kuwa mwaka uliopita Jeshi la Iran lilifanikiwa pia kuinasa ndege ya kisasa ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ-170 huko mashariki mwa nchi.