Wednesday, December 5, 2012

IRAN YAPATA TAARIFA ZA SIRI KWA NDEGE YA MAREKENI ILIYOKAMATWA


Jeshi la ulinzi la Ira limefanikiwa kuchomoa habari zote za siri katika ndege ya kijasusi isiyo na rubani (drone) ya Marekani aina ya ScanEagle iliyonaswa hivi karibuni na jeshi hilo katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
Idara ya Habari ya IRGC imesema kuwa 'drone' hiyo mbali na kufanya ujasusi kuhusu masuala ya kijeshi pia ilikuwa na jukumu la kukusanya habari za shughuli za usafirishaji mafuta katika bandari za Iran.
 Siku ya Jumanne Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran Admeli Ali Fadavi alisema kuwa wataalamu wa jeshi hilo walifanikiwa kushusha chini na kuinasa ndege hiyo ya kijasusi ya Marekani ambayo ilikuwa imeingia katika anga ya Iran ikiongozwa kutoka mbali. Ikumbukwe kuwa mwaka uliopita Jeshi la Iran lilifanikiwa pia kuinasa ndege ya kisasa ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ-170 huko mashariki mwa nchi.

No comments:

Post a Comment