Sunday, March 31, 2013

KILIMO KWANZA NA JEMBE LA MKONO


Baadhi ya majukumu ya kilimo kwanza mpaka mwaka 2015 ni
1. Kuwaendeleza wakulima wadogo na wa kati kuwa wakulima wa kisasa na wa kibiashara.
2. Kuhimiza wakulima wa kati na wakubwa wachangie kwa ukamilifu kufanikisha kilimo kwanza.

Je, mpaka kufikia 2015 hayo yatakuwa yamefikiwa?

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Tanzania
Investiment Centre (TIC), Tanzania Tree Seed Agency (TTSA), The institute of Social Work
(ISW), Business Registration And Licensing Agency (BRELA), The National Institute for
Productivity (NIP), Institute of Finance Management (IFM), The Copyright Society of
Tanzania (COSOTA), Tanzania Institute of Education (TIE), The Mwalimu Nyerere Memorial
Academy na Tanzania Broadcasting Corporation (TBC). Anatarajia kuendesha usaili na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Usaili utafanyika kuanzia tarehe 6 April hadi tarehe 9 April.

Kwa wale wote walioomba ajira angalieni majina yenu ya kuitwa kwenye usaili na maeneo ya kufanyia usail.  MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,134

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.

Tangazo la kiswahili     Tangazo la kiingereza
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 27 Machi, 2013

Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz au Simu; 255-687624975.

UHURU KINYATA THE SECOND YOUNGEST PRESIDENT IN EAC

By Butije Hamisi

Mr Kenyatta will become the second youngest president in the East African Community after Pierre Nkurunziza of Burundi, who is 49.

 President Yoweri Museveni of Uganda is the oldest at 68, followed by Jakaya Kikwete of Tanzania, 63, and Paul Kagame of Rwanda, 55. 

Mr Odinga accepted the court verdict and wished Mr Kenyatta and his team well, one day after the president of the Supreme Court Willy Mutunga read the judgement. The judgment now paves the way for Mr Kenyatta and Mr Ruto to embark on delivering on the promises contained in their campaign manifesto

TAFAKARI: WATAWALA,VIONGOZI & WAPIGAKURA

Na Butije Hamisi, Mwanza
Kila mtu anaweza kuwa mtawala, lakini si kila mtu anaweza kuwa kiongozi. Kuna viongozi wachache sana duniani huku mataifa mengi yakiwa yamegubikwa na watawala.

Hivi wananchi wanaondamana maeneo mboalimbali duniani kwa lengo la kuwaondoa madarakani viongozi au watawala waliowachagua inamaana wakati wanawachagua hawakuwa makini kwa kile walichokuwa wakikifanya?

Ni wazi kuwa wananchi katika mataifa mengi duniani wamekuwa wakipiga kura kuwachagua watawala au viongozi wao, lakini baada ya muda mfupi huanza kulalama na kuwapinga watawala/viongozi waliowapigia kura wao wenyewe. Swali linalonipa ukakasi hapa nio je, inamaana raia wa mataifa mengi duniani huwa ni mambumbumbu katika utashi wao wa kuamua mtawala au kiongozi wao?

Kuna baadhi ya watu wameshika hatamu kwa njia ya mapinduzi na wakatokea kuwa viongozi na wengine watawala, na ilipofika kwenye uchaguzi wachaguaji waliwapa nafasi na baadae kuanza kulalamika na kufanya maandamano ya kuwaondoa madaraka ambayo mengi yao huleta maafa na uharibifu mkubwa wa rasilimali.

Katiba za mataifa mengi duniani zimeweka kinga kwa mtawala au kiongozi aliyechaguliwa na wanachi. wananchi hao wanakuwa hawana uwezo wa kumtoa madarakani mpaka kipindi chake kiishe au waamue kutumia nguvu. Nguvu ambayo imekuwa ikitumiwa na wananchi  wa mataifa mbalimbali duniani ni maandamano.

Swali la kujiuliza tena hapa ni je, kuandamana kwa lengo la kuwaondoa madarakani viongozi tuliowachagua ndio uamuzi makini/sahihi wa kufika matarajio yale tuliyoyatarajia wakati tukiwachagua watawala/viongozi walioko madarakani? Rejea vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa katika chi za kiarabu.

Saturday, March 30, 2013

ARSENAL YAFANYA KUFURU, MAN U YAIBUKA KWA USHINDI MWEMBAMBA

Pichani ni bao lililofungwa na Van Persie lililoipa ushindi Man U wa bao moja dhidi ya Sunderland
Matikeo ya mechi za leo katika ligi kuu ya Uingereza ni  Sunderland 0 - 1 Manchester United, Arsenal 4 - 1 Reading, Manchester City 4 - 0 Newcastle United, Southampton 2 - 1 Chelsea, Swansea 1 - 2 Tottenham, West Ham 3 - 1 West Bromwich Albion, Wigan 1 - 0 Norwich       

RAILA ODINGA AKUBALI KUSHINDWA, AWATAKA WAKENYA KUDUMISHA AMANI



MGOMBEA wa Urais nchini Kenya kwa tiketi ya muungano wa Chama cha CORD Raila Amolo Odinga amekubali kushindwa katika kesi ya kupinga matokeo aliyofungua katika Mahakama ya Juu nchini humo.

Akihutubia taifa hilo muda mfupi uliopita,Odinga amesema kwamba anakubalina na hukumu hiyo iliyosomwa na Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga.

"Nimekubalina na matokeo hayo kwa sababu yakuheshimu Katiba ya Kenya ambayo inasema matokeo ya urais yapingwe katika Mahakama hiyo na maamuzi yatakayotolewa na Mahakama ndiyo ya mwisho"alisema Odiga.

Alisema, "Nilikwenda mahakamani kwa maslahi ya wakenya, hivyo natangaza rasmi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa na kuitakia amani serikali iliyoko madarakani,nitashikiana nao katika kujenga nchi yetu".

Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Mahakama hiyo Jaji Mkuu Willy Mutunga kutoa hukumu ya kesi hiyo na kusema kwamba mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa huru na uwazi na kumfanya  Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto kuchaguliwa   

Wednesday, March 27, 2013

VYUO MBALI MBALI VYA TANZANIA, SIFA ZA UOMBAJI, NAMNA YA KUOMBA, TOVUTI ZA VYUO HIVYO.

 KWA WAOMBAJI WA KOZI MBALIMBALI TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI ZIFUATAZO KWA MSAADA ZAIDI:

Chuo cha ufundi Arusha (ATC).www.atc.ac.tz.
Sifa za mwanafunzi ni kupata angalau (D)katika masomo ya sayansi ambayo ni mathematic,physics,chemistry kwa mwanafunzi wa kike but kwa mwanafunzi wa kiume awe amepata (c) katika masomo mawili kati ya hapo juu baada ya hapo ataitwa katika access course ambayo inachua muda wa miezi miwili na wiki mbili mwanafunzi anatakiwa kupata alama hamsini katika kila somo ambayo ni mathematic,physics ,computer and mechanic gharama za acc
Ess course ni shilingi laki mbili kula na kulala Chuo kwa female only

DAR ES SALAAM INSTUTE OF TECHNOLOGY (DIT) www.dit.ac.tz
Sifa ni nikupata angalau (D) katika masomo yote ya sayansi kwa kila man and woman
Kuna access course kwa muda wa miezi miwili na wiki mbili kwa gharama za sgilingi laki na nusu kulala chuo but kula kila mwanafunzi anajitemea but wanafunzi wataofauru watadhaminiwa na serikali kwa gharama za kulipa shilingi laki mbili na kumi
Course tembelea kwenye website yao hapo juu.

MBEYA INSTUTE OF TECHNOLOGY AND SCIENCE(MIST) www.mist.ac.tz
Sifa kila mwanafunzi aliyefauru angalau (D) Katika masomo ya sayansi
Fomu inapatikana kwa shilingi elfu kumi na tano kwenye tovuti yao hapo juu .
Kuna access course kwa wanafunzi watakachaguliwa kujiunga na chuo kwa muda wa miezi miwili na wiki mbili(2) kwa mwanamke analipa shilingi laki moja na kumi kula anajitemea kwa mwanaume shilingi laki mbili na thelathini kula anajitemea akifauru anakuwa Under government sponsorship scheme atalipa shilingi laki mbili na nusu

MBEGANI FISHERIES DEVELOPMENT CENTRE
Kuna course mbalimbali pale chuoni ,fomu zinapatikana pale chuoni Ada kwa sasa shilingi laki saba kwa mwaka kula na kulala chuoni
Sifa za mwanafunzi kujiunga chuoni ni kupata (D)katika masomo ya sayansi
Kwa ngazi ya cheti muda wa course ni miaka miwili
Kwa mwanafunzi wanachukua diploma sifa za kujiunga ni
Kupata angalau `S`mbili Katika masomo ya sayansi muda wa course ni miaka miwili

VYUO VYA MIFUGO NA MAENDELEO YA UVUVI
Sifa ya kujiunga na vyuo vya mifugo ni kufauru masomo ya sayansi kwa kiwango kisicho pungua points 28 katika kiwango kimoja na kufauru masomo ya sayansi kwa kiwango cha (d) muda wa course ni miaka miwili tu.

Ada sasa ni shilingi laki tatu private laki tisa kwa mwaka kwa ngazi ya cheti na diploma kwa sifa za kujiunga nachuo kwa ngazi ya diploma ni `S` kwa masomo ya sayansi tu maombi kutuma kwa KATIBU MKUU WAZARA YA MIFUGO NA M
AENDELEO YA UVUVI S.L.P.9252 DAR
CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII DAR ES SALAAM
CHUO KINATOA COURSE ZIFUATAZO
Human resource management ngazi ya cheti na diploma kwa sifa ya (d-5)kwa ngazi ya cheti na (s-e)kwa ngazi ya diploma
Social work –course kwa ngazi yha cheti na diploma
Fomu zake ni shilingi elfu ishilini tu tembelea www.isd.ac.tz

CHUO CHA USIMAMIZI WA MAHAKAMA LUSHOTO- TANGA(www.ija.ac.tz)

Kuna course moja tu ambayo ni
Certifacate of Law muda ni mwaka mmoja tu
Sifa ya kujiunga ni kupata (D) Katika masomo ya Arts Kufauru sommo la Engilish ni lazima fomu zinapatikana kwa shilingi elfu kumi na tano tu
Kwa ngazi ya Diploma ni kupata credit 5 za kidato cha nne au kupata japo (E-S)katika masomo ya Arts
Ada ni shilingi milioni moja laki tatu kwa mwaka without accommodation

Tembelea website zifuatazo kwa maelezo muhimu

www.kiu.ac.tz. KAMPALA INTENAL UNIVERSITY
www.mu.ac.tz.Mzumbe University
www.saut.ac.tz ST AUGOSTINO UNIVERSITY
www.chuo cha serikali za mitaa.ac.tz sifa d-5 kwa ngazi ya cheti
www.chuo kishiriki cha sua kilichopo arusha.ac.tz
www.chuo cha kumbukumbu cha mwaliumu nyerere.ac.tz

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
S.L.P 9083 DAR ES SALAAM
Sifa za muhombaji ni kupata japo d ya somo la biology kwa ngazi ya cheti kufauru mathematic ni sifa ya ziada barua iwe na picha tatu na cheti cha kuzaliwa kwa ngazi ya cheti kupata angalau `S` katika masomo ya sayansi
Kuna course kama ifuatayo
Clinical officer
Hearth officer
Laboratory officer
Assistance officer of clinical officer
Dental officer:

SIRI KUUAWAWA KWA ZITTO KABWE YAFICHUKA.

YADAIWA ILIPANGWA ANYWESHWE SUMU HOTELINI, DK SLAA ATAJWA KUMTUMA SAANANE KUMMALIZA, MWENYEWE AKANUSHA, ASEMA NI SIASA CHAFU
 TISHIO la kuuawa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, sasa limechukua sura mpya, baada ya kuibuika kwa madai mapya kuwa Bosi wake, Dk. Willbrod Slaa, alipanga njama za kumuangamiza, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Duru za habari zinaeleza kuwa Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, anadaiwa alitaka kuuawa kwa sumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Slaa, ambaye alimtumia kada na Mjumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Ben Saanane, kutekeleza mpango huo.

Habari zinadai kuwa tukio hilo lilipangwa kutekelezwa Mei mwaka jana, katika Hoteli ya Lunch Time, iliyoko Mabibo External, jijini Dar es Salaam.

Kwamba Zitto alilengwa kuuawa kwa kuwekewa sumu kwenye kinywaji chake wakati akiwa kwenye mazungumzo na baadhi ya makada vijana wa chama hicho katika Hoteli ya Lunch Time.

Mmoja wa watu waliokuwa katika tukio hilo amelieleza MTANZANIA Jumatano kuwa Zitto alinusurika baada ya aliyetumwa kumuwekea sumu hiyo kuidondosha na hivyo kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo.

Anamtaja mtu aliyetumwa kumuua Zitto kuwa ni Ben Saanane, ambaye aliangusha karatasi ya nailoni iliyokuwa na ungaunga unaosadikiwa kuwa sumu na kuonekana kwa watu waliokuwa eneo hilo, akiwemo Zitto mwenyewe pamoja na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano, Shonza alikiri kutokea kwa tukio hilo kwa kueleza kuwa yeye na Mwampamba walihoji kilichokuwa ndani ya nailoni ile, ambacho kilionekana wazi kuwa ni unga unga ni nini, ambapo Saanane alikiri kuwa ilikuwa sumu ambayo alipewa na Dk. Slaa, ili amuwekee Zitto.

Shonza alidai kuwa siku ya tukio, yeye na Zitto walikuwa wamekaa meza moja na Saanane ambaye mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa bandeji aliyowaeleza kuwa aliifunga kutokana na maumivu ya mkono.

Alisema wakiwa katika maongezi, huku Saanane akionyesha kuzidiwa na kilevi alichokuwa amekunywa, alitoa bahasha ya kaki yenye fedha ili alipie gharama za vinywaji vya wote ambayo ilidondoka na ndani yake ikatoka karatasi ndogo ya nailoni  ikiwa na unga mwekundu.

Kwa mujibu wa Shonza, Saanane alipobanwa aeleze unga ule ulikuwa nini, awali  alidai ni kilevi aina ya kuberi, huku akiwataka wasiifungue nailoni hiyo, jambo ambalo Mwampamba alilikataa na kulazimisha ifunguliwe pale pale.

“Kwa hasira Ben alitaka arudishiwe ile karatasi, lakini, Mwampamba aliondoka nayo, usiku huo huo Saanane alimtafuta Mwampamba hadi nyumbani kwake akidai apewe mzigo wake.

“Mwampamba alimwambia atampa mzigo wake kwa sharti moja tu la kusema ukweli kuhusu kilichomo ndani ya nailoni hiyo na hapo ndipo Ben alipokiri kuwa alipewa mzigo huo ambao una unga unga wenye sumu na Dk. Slaa, ili amuwekee Zitto kwa sababu amekuwa akimsakama ndani ya vikao vya chama.

“Huo ndiyo ukweli ambao nitausema popote, sasa kama Ben alitudanganya kwa kumsingizia Dk. Slaa hiyo ni juu yao wenyewe,” alisema Shonza.

Shonza alisema hali hiyo iliwaogofya na kuanza kuwa makini katika mapito yao na kuongeza kuwa Zitto bado yuko Chadema kwa sababu ana roho ngumu, mvumilivu na mkomavu wa kisiasa, anayeweza kukabiliana na mambo ya hatari.

Dk. Slaa alipoulizwa na MTANZANIA Jumatano kuhusu madai hayo, alisema hilo ni kosa la jinai, ambalo kama anatuhumiwa kulifanya anapaswa kushtakiwa kwenye vyombo vya dola badala ya tarifa hizo kupelekwa katika vyombo vya habari.

“Usipende kutumiwa na watu, lakini aliyekutuma anajua amekutuma kwa sababu gani. Sasa nitakujibu, hivi suala la kuua si ni jinai? Sasa suala la jinai linapelekwa kwenye vyombo vya dola au kwenye vyombo vya habari ?.

Huyo aliyesema yuko Chadema au yuko wapi? Aliyesema hakwenda polisi ?.

Aliyetaka kuuawa hakwenda pia? Sasa ninyi media mmekuwa nani?

“Wa kumuuliza suala hili ni Saanane mwenyewe au Shonza, wangekuwa na nia njema wangekwenda polisi au Zitto mwenyewe angekwenda polisi kushitaki kwa kutaka kuuawa,” alisema Dk. Slaa.

Naye Saanane ambaye amefanya mahojiano na MTANZANIA Jumatano kuhusiana na mambo mbalimbali mabaya ambayo yamekuwa yakielekezwa kwake, akizungumzia madai hayo alisema madai hayo hayana ukweli wowote, bali yanaibuliwa sasa na mahasimu wake kisiasa kwa lengo la kutaka kumshusha baada ya majaribio mengi dhidi yake kushindwa.

“Kwanza siku ambayo wanasema tulikuwa wote mimi sikuwa huko, nashangaa na haiingii akilini kwamba mimi niende hadi Temeke (kwa Mwampamba) tena usiku wa manane kwa ajili ya kufuata sumu ya kuulia panya.

“Hizi ndizo siasa halisi za maji taka, kuliko nipange njama za kuua mtu kwa malengo ya kisiasa, ni bora niache siasa. 

Ni mwendawazimu pekee atakayeweza kuamini tetesi hizi za ovyo kabisa zinazofanywa na vijana walioshindwa kujenga hoja za maana kwenye majukwaa,” alisema Saanane.

Aliwaonya watu wanaohasimiana naye kisiasa kuacha kumchafua Dk. Slaa kwa kutumia jina lake katika mambo wanayomtuhumu, kwa kile alichoeleza kuwa ni dhambi kubwa kutunga uongo na kuusambaza ili kutafuta huruma ya umma wa Watanzania.

“Nadhani lengo lao hapa ni kumchafua Dk. Slaa kwa tuhuma hizi za uongo zilizotolewa kwa mara ya kwanza na vijana waliotimuliwa Chadema kwa kukisaliti chama na baadaye kuhongwa na makada na viongozi wa CCM ambao wamejiunga nao sasa.

“Sasa kwa tuhuma hizo, kwa nini wasiripoti polisi, inaingiaje akilini mtu kupanga njama kubwa kiasi hicho halafu ukae kimya tu,” alisema Saanane.

CHANZO:  http://www.mtanzania.co.tz

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUDUMISHA AMANI NCHINI



Na Shaffiru Makosa & Muharami Matenga- kigoma

Wakati jitihada mbalimabli zikiendelea kufanywa na serikali kwa lengo la kudumisha amani  na upendo miongoni mwa wanajamii ya watanzania Kaimu  sheikh mkuu wa mkoa wa Kigoma wa baraza kuu la waislamu Tanzania bakwata Alhaji Hassan Kibulwa  ameunga mkono hatua hiyo ya  kudumisha amani na upendo nchini kwakuwataka viongozi wa dini kutekeleza maazimio mbalimbali ya vikao vya  mabaraza ya mahusiano mema vinanavyo shirikisha viongozi wa dini zote kwa lengo la  kudumisha  amani na upendo ha pa nchini.

Alhaji kibulwa ameyasema hayo katika kikao maalum cha baraza kuu la waislamu Tanzania bakwata mkoa wa kigoma kilichoshirikisha viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali kwa shabaha ya kujadili mustakbali wa amani ya mkoa huu  ikiwa ni pamoja na kutafuta ufumbuzi wa  migogoro ya kidini  inayoendelea kushika kasi  katika baadhi ya maeneo hapa mkoani Kigoma .insert ….

Alhaji Kibulwa amekemea tabia ya baadhi  viongozi wa dini wa kiislamu wanaotumia maandamano kama silaha ya  kuishinikiza serikali kutekeleza madai yao jambo ambalo ni kwenda kinyume  kabisa na mafundisho ya mtume muhamadi (s.a.w)

Licha ya shekhe kibulwa kuwataka viongozi hao wa  dini ya kiislamu  na wakiristu kutataua changamoto  zinazohatarisha mahusiano ya waumini wao  kwa njia ya kidiplomasia   pia akatoa wito kwa viongozi hao kujishughulisha katika kutafuta ufumbuzi wa chanagamoto za kimaendeleo kwa waamini wao ikiwemo za  kielimu  na kiuchumi badala ya kujikita katika masuala ya kiimani pekee.

Kufuatia hatua hiyo ya kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kigoma  ya  kuunga mkono zoezi la kudumisha amani nchini baadhi ya viongozi  hao wa dini  katika  mkutano huo wakatilia mkazo juhudi hiyo kwakulitaka baraza la waisalamu Tanzania bakwata kukaza buti katika kushughulikia harakati za kimaendeleo nchini ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha waumini wake bila kujali mipasuko ya kimadhehebu.

Thursday, March 21, 2013

WAFUASI 52 WA SHEIKH PONDA WAFUNGWA JELA MWAKA MMOJA.

Wafuasi wa Ponda wakipanda kalandinga kwenda jela baada ya kuhukumiwa jela  mwaka mmoja 
WAKATI kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, ikiendelea katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu wafuasi wake 52 kati ya 53 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya maandamano haramu wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimwachia huru mshtakiwa mmoja, Waziri Omar Toy, ambaye alikuwa mshtakiwa wa 48 katika kesi hiyo baada ya kuridhika
kuwa hana hatia kutokana upande wa mshtaka kushindwa kuthitibisha mashtaka dhidi yake.

Wafuasi hao wa Ponda walihukumiwa adhabu hiyo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikiana na hatia katika makosa matatu yaliyokuwa yakiwakabili kati ya manne.

Wafuasi hao wa Ponda walikamatwa Februari 15 wakidaiwa kufanya maandamano haramu kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa lengo la kumshinikiza aondoe zuio la dhamana dhidi ya Ponda na mwenzake, Mukadamu Swalehe, wanaokabiliwa na kesi ya uvamizi wa kiwanja cha Chang’ombe Markazi.


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alisema kuwa baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za pande zote pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ameridhika, kuwa upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka matatu dhidi ya washtakiwa hao.
“Katika kosa la kwanza ninawahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela, na kosa la pili pia mwaka mmoja jela na tatu mwaka mmoja jela. Adhabu zote
zinakwenda kwa pamoja.”alisema Hakimu Fimbo.

Aliyataja mashtaka hayo ambayo washtakiwa walipatikana na hatia kuwa ni shtaka la kwanza la kula njama za kutenda makosa, la pili, kufanya maandamano yaliyozuiwa na Jeshi la Polisi na la tatu kufanya mikusanyiko haramu na kusababisha uvunjifu wa amani.

Hata hivyo Hakimu Fimbo alisema kuwa katika shtaka la nne la uchochezi wa kutenda kosa lililokuwa likiwakabili washtakiwa wanne, upande wa mashtaka umeshindwa kulithibitisha.
“Mahakama imeridhika na ushahidi uliwasilishwa na upande wa mashtaka kuwa umethibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48.”, alisema Hakimu Fimbo na kuongeza: “Hivyo mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48, katika shtaka la kwanza, la pili na la tatu, na katika shtaka la nne, mahakama imeona kuwa washtakiwa hawana hatia.”

Tuesday, March 19, 2013

SAMATA NA ULIMWENGU WATUA NCHINI KUIKABILI MOROCCO

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania,(Taifa Stars) Mbwana Samatta (kulia) akijaribu kumtoka beki wa timu Cholo wakati wa mazoezi hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.
Ujio wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mchaliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti kambini leo asubuhi.
Wachezaji John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao walikuwa Liberia na timu yao ya Azam walitarajiwa kuripoti kambini leo alasiri. Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia nayo wenzao kuwa imejaa.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Kim Poulsen leo inaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Mazoezi hayo yataanza saa 9 alasiri.

Monday, March 18, 2013

MSAFARA WA RAIS WAUA ASKARI WA USALAMA BARABARANI DAR.


"Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.

Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:

Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.

Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.

Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu"

CHANZO: JAMII FORUM

MGOGORO WA KAFULILA NA MBATIA WAKOMA: KAFULILA AREJEASHWA KUNDINI BAADA YA KUOMBA RADHID

David Kafulila
Na Magreth Magosso, Kigoma

Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini, David Kafulila wa chama cha NCCR-Mageuzi ameomba radhi kwa chama chake, baada ya kugundua makosa yake yaliyopelekea kutaka  kuvuliwa ubunge na hatimaye kwenye chama hicho.

 Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Taifa  wa chama NCCR-Mageuzi Samweli Ruhuza wakati akihutubia  maelfu  ya wakazi wa kata ya  Nguruka kwenye mkutano wa hadhara wa kuhamasisha wananchi wajiunge na chama hicho,ambao  ulifanyika  viwanja vya shule ya msingi Nguruka   na kubainisha  utovu wa nidhamu alioufanya mbunge huyo na mkakati wa kumaliza tofauti hizo ili kukiimarisha chama.

"ule mgogoro  baina ya  Mwenyekiti Mhe.Mbatia na mbunge wenu  hivi sasa haupo, na wanafanya kazi kwa kushirikia  ili kujenga chama chetu kiweze kuwa imara na chenye nidhamu" amesema  Ruhuza huku wanachama wapya 153 wakichukua kadi kujiunga chama hicho.

Ruhuza alidai kuwa Mhe.Kafulila ametafakari na kugundua kuwa alichokuwa anakifanya si sahihi na ili kumaliza nongwa akamua kuomba radhi sanjari na  masharti  ikiwa na tija ya kutimiza vigezo fulani  ambao kwa hivi sasa ameshakamilisha kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama.

Aidha halmashauri kuu ya chama hicho kilikaa katika kikao chake mwezi wa tisa mwaka jana na kupokea ombi la msamaha wa Mhe Kafulila na kukubali ombi hilo la kumsamehe,huku halmashauri kuu itakaa tena kikao mwezi wa nne tarehe sita ili kuweka bayana uhalali wa kurudishwa kundini kwa mbunge huyo.



Amedai kuwa, lengo la uongozi wa chama kutaka kumfukuza uanachama Mhe.Kafulila halikuwa la kiutashi wa maslai binafsi la! bali ni kutaka kujenga nidhamu ndani ya chama  ambayo ndio msingi  wa awali   kwa miaka kenda hivyo hakuna mwanachama anayeweza kuwa juu ya sheria ya katiba ya  chama hata siku moja na ikifika hatua hiyo ni kheri ajifuke mwenyewe.


POLISI WAPEKUA OFISI ZA CHADEMA, LWAKATARE AFIKISHWA MAHAKAMANI

Wakati Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo, jana mchana ofisi za makao makuu ya chama hicho zilipekuliwa na polisi na kuondoka na nyaraka mbalimbali.
Tukio hilo lilitokea jana ikiwa ni mwendelezo wa upelelezi wa tuhuma zinazomkabili Lwakatare ambazo zinazomhusisha na picha ya video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii. Lwakatare alikamatwa Jumatano iliyopita akihusishwa na picha hiyo iliyomwonyesha Lwakatare akiwaelekeza watu ambao hawakuonekana, kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani au uhalifu.
Polisi hao wakiwa na Lwakatare na mmoja wa mawakili wake, Nyaronyo Kicheere walikwenda kwenye ofisi za Chadema saa 9.00 alasiri kwa ajili ya kufanya upekuzi.
Upekuzi huo uliendeshwa zaidi kwenye ofisi za Lwakatare kwenye Makao Makuu ya Chadema yaliyoko Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Upelelezi wa kesi hiyo unaongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Obadia Jonas ulikuwa na lengo la kupata hati zenye mwandiko wa Lwakatare ili kufananisha na nyaraka mbalimbali walizonazo polisi. Kwa nyakati tofauti, Nyaronyo Kicheere na Ofisa Habari Mwandamizi wa Chadema, Tumaini Makene walithibitisha juu ya upekuzi huo.
CHANZO: MWNZANCHI

Saturday, March 16, 2013

ROONEY AIPAISHA MANCHESTER UNITED …ARSENAL YAICHINJA SWANSEA, LIVERPOOL YAPIGWA 3-1




RIO GRAND ... Ferdinand beats Noel Hunt to the ball
MANCHESTER UNITED wamezidi kujikita kileleni mwa Ligi kuu ya Uingereza baada kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Reading.
Bao hilo pekee lilikuja dakika ya 23 kupitia kwa Wyane Rooney.
Mpira ulianzia kwa Rio Ferdinand aliyepanda na mpira huku akiichambua ngome ya Reading kabla ya kumpa pasi Rooney aliyepiga mkwaju uliombabatiza Pearce na kwenda wavuni.
WAY TO GO ... Rooney opens the scoring after his strike deflects in off Alex Pearce
Rooney akifunga goli pekee
Dakika ya 48 Reading walinyimwa penalti ya wazi baada ya Vidic kumsukuma Mariappa kwenye kisanduku cha hatari lakini kwa mshangao wa wengi refa Mason akauchuna.
Van Persie akakosa nafasi ya kufunga bao la msimu katika dakika ya 90 baada ya kwenda hewani na kuruka tik tak kuunganisha krosi ya Kagawa lakini shuti lake likaenda pembeni.
ASH 'N BURN ... Ashley Young goes down under a challenge from Reading keeper Stuart Taylor
Heka heka langoni mwa Reading
Katika michezo mingine Arsenal iliichapa Swansea 2-0 kupitia magoli ya Nacho Monreal na Gervinho.
Liverpool ikafungwa 3-1 na Southampton huku Aston Villa ikiibuka na ushindi wa 3-2 kwa QPR.
Nayo Stoke City ikiwa nyumbani ikatoka sare ya 0-0 na West Bromwich Albion.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili hii kati Sunderland na Norwich, Tottenham dhidi ya Fulham, Chelsea ikiikaribisha West Ham huku Wigan ikimenyana na Newcastle.

Thursday, March 14, 2013

POLIS KIGOMA WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUSAMBARATISHA MAANDAMANO YA MADEREVA WA BODABODA

Na Magreth Magosso,Kigoma.
 
Polis Mkoani Kigoma wamelazimika kutumia Mabomu ya machozi ili kuwatawanya waendesha  Bodaboda wa  Manispaa ya  Kigoma Ujiji, baada ya kufanya maandamano  ya kutaka askari wa barabarani wasitumie nyadhifa zao kwa maslai yao binafsi.
 
Kauli hiyo imethibitishwa na Mwenyekiti wa waendesha Bodaboda Fikirini Shaban eneo la maweni, kudai kuwa,askari hao wana tabia ya kuwasimamisha waendesha bodaboda si kwa tija ya kuwakosoa na kuwaelimisha kwa makosa husika, bali hutaka kiasi cha fedha kuanzia 10,000 hadi sh.5,000  ili uendelee kufanya kazi,la ukikataa kusimama watakuandama kwa kufukuzana nao barabarani hali inayosababisha ajali zisizo tarajiwa.
“Baadhi ya abiria hukataa kuvaa kofia ,lakini askari akikusimamisha na ukisimama wanatoza fedha isiyo na tija kwa serikali huweka mifukoni mwao jana ajali ilitokea  na kujeruhi watu watatu kisa hakusimama baada ya askari kumsimamisha kwa kuhofu kutolewa  sh.10,000 ukibana sana unatoa 5,000 eti ya mafuta tena hakuna risiti” alibainisha  Kaopa Denis mwendesha pikipik.
Mganga Mkuu wa Kigoma Leonard Subi alikiri Hospitali yake  jana ilipokea majeruhi wa ajali hiyo na kubainisha kuwa, waliolazwa hadi sasa wapo watatu ambao hali zao si za kuridhisha.
 
Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Dismas Gapikisusi alidai kuwa,tukio hilo bado linafanyiwa mkakati wa kuweza kulitolea jibu maalum na kumtaka mwandishi wa gazeti hili asubiri siku wandishi wa habari watakapoitwa ili abainishe ukweli wa mambo.
Wakati huohuo baada ya waendesha bodaboda kufanya mandamano hayo sanjari na kutupa   jaketi za kuakisi mwanga kituo cha polisi kati Kigoma, Waendesha pikipiki wanne wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Kigoma kwa kosa la kufanya fujo polisi leo.

Sunday, March 10, 2013

BASI LA KILIMANJARO LAPATA AJALI LEO

.
..
SOURCE: http://jumamtanda.blogspot.com  

BASI LA KILIMANJARO LAPATA AJALI LEO

.
..
SOURCE: http://jumamtanda.blogspot.com  

MWANAFUNZI AUA WATU WA 3 NA KUMI MAHUTUTI

 Na Magreth Magosso,Kigoma

Polisi Mkoa wa Kigoma linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha sita  Stanford Richard (30) mkazi wa kijiji cha Bitale wilayani humo, kwa  kufanya mauwaji ya watu watatu na kujeruhi kumi  ambapo majeruhi nane wako mahututi katika hospitali ya Mkoa  Maweni .
Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa Dismas Gapikakisusi  kigoma ujiji jana  alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari juu ya tukio hilo ambalo ni janga  kwa kijiji cha Bitale na mkoa mzima.
Gapikakisusi alibainisha kuwa, chanzo cha mauwaji hayo  ni sintofahamu, ingawa kijana huyo inasadikiwa baada ya kumaliza masomo yake sekondari kijiji hapo, alianza kuingiwa na hali ya kurukwa na akili na hadi jana kufanya mauwaji ya  Sebastian Julius(22) Rudia Richard (71) n,Ezema Lazaro(65)nyakati za asubuh.
" majeruhi wapo nane na hali zao ni mbaya hapo maweni ni pamoja na Pendo Jumbe(35),Jumbe Budio(50),Richard Manase(60),Rith James(55) na wengine watano huku majeruhi wawili wamepatiwa matibabu na wamerejea majumbani hamuwezi kumuona huyo kijana kwani hali yake ni tete" alidai Gapikakisusi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho alisema kuwa kijna huyo alianza kuwakata mapanga baba na mama yake kisha kuhamia myumba ya jirani kwa Jumbe Budio na kuishambulia familia yake  kwa kuwajeruhi kwa kutumia dive la gari na kipande cha nondo chenye mm 18  akiwemo mtoto wa shule ya msingi na kuhamia mtaani kuendeleza mashambulizi .
Baadhi ya majeruhi Pendo Jumbe na Dotto Issa wakiugulia maumivu makali huku wakiongea kwa kujivutavuta walibainisha kwamba,walishtukizwa na kipigo cha kitu kizito sehemu za kichwa hali iliyowapoteza fahamu na kujikuta wapo hospitali huku mama wa kijana huyo akiri kijana wake huwezi kuamini kama ni chizi kutokana na ukimya wake.
Mganga Mkuu wa Mkoa Leonard Sub akiri kuwepo kwa maiti hizo na majeruhi wakati  mkazi wa bitale  Aziza alipoulizwa juu ya tukio hilo alidai kuwa, ilikuwa saa moja za magharibi ndipo walisikia kelele za jamii kuwa  watu watatu walikufa  kwa kukatwakatwa na mapanga na wengine kujeruhiwa sehemu za kichwani  huku akidai kijana huyo ana tatizo la akili  baada ya kumaliza  kidato cha  sita kwenye moja ya shule za kata  kijijini hapo.

WANAFUNZI WA SHAHADA YA ELIMU NA FILOSOFIA SAUT WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA




Wananfunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya elimu na filosofia SAUT wakiangalia makaburi ya wazazi wa Baba wa Taifa Mwalim Nyerere katika makumbusho ya Mwalim Nyerere- Butiama





Wananfunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya elimu na filosofia SAUT wakiwa katika jengo ambalo lina kaburi la Baba wa Taifa katika makumbusho ya Mwalim Nyerere- Butiama






Muhadhiri wa chuo cha SAUT Mr. Mugishagwe akitoa amelekezo kwa wanafunzi wake wakiwa katika makumbusho wa  Mwalim Nyerere Butiama





Radio alokuwa akiitumia Baba wa Taifa Mwalim Nyerere. Inauzito wa kilogram 20.

Wananfunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya elimu na filosofia SAUT wakiangalia  vivutio vya kitalii katika makumbusho ya Mwalim Nyerere- Butiama

Wananfunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya elimu na filosofia SAUT wakiangalia  vivutio vya kitalii katika makumbusho ya Mwalim Nyerere- Butiama

Friday, March 8, 2013

MAMA SALMA KIKWETE ATOA UJUMBE KWA WANAWAKE KUPITIA FACEBOOK


MKE wa Rais Mama salma Kikwete ametoa salam zake kwa wanawake wote duniani na kuwatakiwa maisha mema na yenye baraka katika.Mama Salam alitoa salam hizo kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alisema "Leo ni siku ya wanawake Duniani,ni siku ya kujitazama kama Taifa juu ya hali ya wazazi hawa na walezi wa Taifa hili".

"Ni siku ya kujipima na kutathimini namna gani, wanawake wamewezeshwa kujitambua na kushirikishwa katika mipango ya maendeleo ya jamii yetu. Tunapofikiri kama Taifa ni namna gani tunaweza kujikomboa katika Umasikini tulionao ni lazima mipango hiyo iende sambamba na mipango na mikakati ya ukombozi kwa wanawake wa Taifa hili"aliongeza Mama Salma.

Maadhimisho hayo yamefanyika duniani kote ambapo Tanzania yalifanyika kila mkoa, huku jijini Mwanza yakifanyika katika viwanja vya Nyamagana.