David Kafulila |
Na Magreth Magosso, Kigoma
Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini, David Kafulila wa chama cha NCCR-Mageuzi ameomba radhi kwa chama chake, baada ya kugundua makosa yake yaliyopelekea kutaka kuvuliwa ubunge na hatimaye kwenye chama hicho.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Taifa wa chama NCCR-Mageuzi Samweli Ruhuza wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa kata ya Nguruka kwenye mkutano wa hadhara wa kuhamasisha wananchi wajiunge na chama hicho,ambao ulifanyika viwanja vya shule ya msingi Nguruka na kubainisha utovu wa nidhamu alioufanya mbunge huyo na mkakati wa kumaliza tofauti hizo ili kukiimarisha chama.
"ule mgogoro baina ya Mwenyekiti Mhe.Mbatia na mbunge wenu hivi sasa haupo, na wanafanya kazi kwa kushirikia ili kujenga chama chetu kiweze kuwa imara na chenye nidhamu" amesema Ruhuza huku wanachama wapya 153 wakichukua kadi kujiunga chama hicho.
Ruhuza alidai kuwa Mhe.Kafulila ametafakari na kugundua kuwa alichokuwa anakifanya si sahihi na ili kumaliza nongwa akamua kuomba radhi sanjari na masharti ikiwa na tija ya kutimiza vigezo fulani ambao kwa hivi sasa ameshakamilisha kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama.
Aidha halmashauri kuu ya chama hicho kilikaa katika kikao chake mwezi wa tisa mwaka jana na kupokea ombi la msamaha wa Mhe Kafulila na kukubali ombi hilo la kumsamehe,huku halmashauri kuu itakaa tena kikao mwezi wa nne tarehe sita ili kuweka bayana uhalali wa kurudishwa kundini kwa mbunge huyo.
Amedai kuwa, lengo la uongozi wa chama kutaka kumfukuza uanachama Mhe.Kafulila halikuwa la kiutashi wa maslai binafsi la! bali ni kutaka kujenga nidhamu ndani ya chama ambayo ndio msingi wa awali kwa miaka kenda hivyo hakuna mwanachama anayeweza kuwa juu ya sheria ya katiba ya chama hata siku moja na ikifika hatua hiyo ni kheri ajifuke mwenyewe.
No comments:
Post a Comment